Na John Marwa
TIMU ya Wasichana (U18) ya Zanzibar imeanza vibaya mashindano ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA U18 baada ya kukubali kipigo cha mabao (3-0) kutoka kwa Uganda.
Bao la tatu limefungwa dakika 83 na Phionah Nabulime kwa mkwaju wa penalti baada ya kuchezewa rafu na mabeki wa timu ya Zanzibar.
Mechi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano hayo Uganda aliifunga Ethiopia bao 1-0, leo ameifunga timu ya Visiwani Zanzibar, uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam.
Dakika 45 ya kipindi cha kwanza kilikamilika sio Uganda wala Zanzibar waliofanikiwa kutikisa nyavu zao mwenzake.Mchezo ulikuwa wa kasi Zanzibar hawakuwa na mipango mizuri ya kumalizia kwenye safu yake ya ushambuliaji huku safu ya ulinzi kuonekana makini kuzuia.
Kwa upande wa Uganda walifika mara kadha kushambulia langoni kwa Zanzibar kwa kutengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia.Dakika ya 2 na 26 Uganda kupitia mchezaji wake Shamusa Najjuma alipiga shuti na kipa wa Zanzibar, Aisha Said amefanya kazi nzuri kwa kuucheza mpira na kutoka nje.
Kikosi cha Zanzibar:Aisha Said, Amina Ramadhani, Wiggo Magoma, Rahma Nassoro, Rukia Laizar, Agness Millanzi, Mwamvita Muba, Hawa Juma/ Fatma Juma, Saada Said, Fatma Bakar na Anna James/ Zainabu Nassad.
Uganda:Sharon Kaidu, Desire Katisi, Brenda Munyana, Agnes Nabukenya, Shamusa Najjuma/ Allen Nassaazi, Krusum Namutebi, Sharifa Nakimera, Patricia Nanyanzi, Phionah Nabulime, Kamiyati Naigaga/Patricia Nayiga na Patience Nabulobi.
Michuano hiyo itaendelea kesho kutwa (Jumapili) mechi ya kwanza itacheza saa 9:00 alasiri, kati ya Ethiopia dhidi ya Burundi, mchezo wa pili Tanzania ni wenyeji watawakaribisha ndugu zao kutoka Visiwani Zanzibar, saa 12:00 jioni mechi zote zitacheza Azam Complex.
No comments:
Post a Comment