HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 01, 2023

Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe Wahimizwa Kuchangia Ujenzi Hosteli ya Wanafunzi wa Kike Ndaki ya Mbeya

Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe, wamekaribishwa kuchangia ujenzi wa hosteli ya Wanafunzi wa kike Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya ambapo harambee ya ujenzi huo ilizinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera Mei Mwaka huu.


Hayo yamesemwa Juni 30, 2023 na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam( DVC ARC) Dkt. Eliza Mwakasangula alipotembelea Banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika maonesho ya 47 ya Biadhaya ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.

Dk. Mwakasangula amesema kuwa Wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu Mzumbe wanaombwa na kuhimizwa kuchangia ujenzi huo kwani hatua hiyo ni ya kizalendo kwa Taifa na ni ukarimu kwa kurudisha huduma kwa jamii kwa kusaidia watoto wa kike kusoma na kuishi katika mazigira mazuri. Alisisitiza

Licha ya kuwakaribisha wanafunzi hao, Dkt. Mwakasangula pia amewaomba wananchi kwa ujumla kuchangia ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike katika kupitia control namba 994180331310

Akiwa katika Banda hilo, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Dkt. Mwakasangula wamewakaribisha wananchi kwa ujumla kwenda kufanya udahili kwa wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo wa 2023/2024.

"Tunawakaribisha kupata huduma mbalimbali, tunadahili wanafunzi kwa ajili ya kujiunga na Program zetu Chuo Kikuu Mzumbe kwa ngazi ya Shahada za awali kwa wale waliomaliza kidato cha nne, kidato cha Sita na hata waliomaliza muda mrefu." Amesema Dkt Mwakasangula

Amewakaribisha watu mbalimbali kutembelea Banda la Chuo Kikuu Mzumbe ili kupata taarifa mbalimbali za Chuo pamoja na kufahamu Chuo kinafundisha masomo yanayo husiana na Biashara, Sheria, Masomo ya Utawala, Uhasibu, Sayansi na Teknolojia

Chuo Kikuu Mzumbe kina Kampasi tatu ambazo ni Mororgoro(Makao Makuu), Mbeya na Dar es Salaam ikiwa na Kituo cha Tegeta wanapotoa shahada za awali.

Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam (DVC ARC) Dkt. Eliza Mwakasangula akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye banda la Chuo na kuangalia huduma mbalimbali zinatolewa na Chuo hicho katika maonesho yanayoendelea katika Viwanja vya sabasaba.

 

 Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam( DVC ARC) Dkt. Eliza Mwakasangula(kulia) akiangalia Moja wapo ya bidhaa zilizotengenezwa na Mercy Mwambe , Mwanafunzi wa Masomo ya Shahada ya Uongozi wa Biashara katika Ujasiliamali na Ubunifu.(BBA EIM)

No comments:

Post a Comment

Pages