Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka Madereva Pikipiki
(Bodaboda) kufanya shughuli zao za usafirishaji kwa kuzingatia taratibu
na sheria za usalama barabarani ili kuepukana na madhara yanayoweza
kujitokeza.
DC
Mpogolo ameeleza jijini Dar es Salaam wakati akizungumza Kwa Niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano uliowakutanisha madereva
bodaboda kutoka maeneo mbalimbali nchi katika uzinduzi wa mfumo tambuzi
wa data base wenye lengo la kuwasajili madereva hao kutambuliwa kwa
haraka katika maeneo yao.
Amebainisha
kuwa ni vyema wakabadilika sambamba na kufata taratibu za usalama
barabarani Ili waweze kuepukana na changamoto ya kuchukuliwa hatua za
mara Kwa mara kutokana na kukiuka sheria.
"Mhe
Rais anawathamini na kutambua kazi munazozifanya kwani watu wengi
wanapata ajira kwa kuuza pikipiki kwa wingi lakini pia mama Lishe
kuwahudumia katika kuwapatia chakula"amesema Mpogolo
Amesema
kuwa wanazipata riziki Kwa kuwa wanafanya shughuli za usafirishaji
kutoka kituo kimoja mpaka cha pili hivyo jukumu lao kama wanataka amani
nivyema wakabadilika.
Aidha
amesema kuwa jiji la Dar es salaam limedhamiria kuweka vituo vya
bodaboda katika maeneo ya jiji hilo ili waweze kutambulika kwa urahisi
jambo ambalo pia litasaidia kuongeza mapato.
Awali
akielezea Mfumo wa Utambuzi wa waendesha pikipiki Mratibu wa Mfumo wa
Utambuzi UCC Elisha Masasi amesema kuwa malengo yao ni kuondoa na
kuwadhibiti vishandu ambao wamekuwa wakifanya Madereva kuonekana hawafai
Kwenye Jamii.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Madereva Bodaboda
na Bajaj Dar es Salaam( SHIVYAMAPIDA), Michael Liganga amemuomba DC
Mpogolo kuwaongezea idadi ya vituo madereva bodaboda na kuwatatulia
chanagamoto ya kupata vitambulisho ili waweze kuondokana na adha ya
kupata leseni.
Nae,
Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Said Chenje amemuhakikishia DC huyo
watafanya kazi kwa ukaribu na Jiji la Dar es Salaam na Jeshi la Poisi
Usalama Barabarani ili madereva Bodaboda waweze kufauata kutii sheria
hizo.
No comments:
Post a Comment