HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 25, 2023

TANZANIA YAICHAKAZA BURUNDI (CECAFA U18)

Na John Marwa


TIMU ya Taifa ya Tanzania ya wasichana U 18 imeanza vizuri kwa kuibuka na ushindi wa mabao (3-0) katika mashindano ya kuwania ubingwa kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Tanzania ni wenyeji wa mashindano hayo yaliyoanza rasmi leo, katika viwanja vya Azam Complex jijini Dar es Salaam na kuibuka na ushindi huo kwa kumfunga Burundi, katika mchezo huo wa ufunguzi. 


Timu zote zilifanya vizuri katika kipindi cha kwanza na timu hizo kushindwa kupata matokeo katika dakika 45 za kipindi hiko.


Kipindi cha pili Tanzania ilianza mpira wa kasi kwa kushumbulia mara kwa mara katika lango la Burundi na dakika ya 64 ikajipatia bao la kwanza likifungwa na Winifrida Gerald kwa mkwaju wa penalti baada  kipa wa Burundi kudaka miguu ya Zainabu Mohammed badala ya mpira.


Dakika ya 71 Zainabu Mohammed alikosa bao la wazi baada ya kushindwa kuweka mpira kambani akiwa anatazamana na nyavu, Sarah Joel ,super sub' ilimchukua  17 kuiandikia Tanzania bao la pili dakika ya 90 ya mchezo na kuifanya Tanzania kuongoza kwa mabao 2 bila.


Wakati watazamaji wakiamini mchezo huo umemalizik dakika ya 90+ Aisha Juma aliweka kambani bao la tatu kwa mpira mrefu uliomshinda mlinda lango wa Burundi Amissa Inarukundo


Kikosi cha Tanzania:Husna Zuber, Noel Patrick,  Hasnath Linus,Joyce Fred, Winifrida Gerald,  Ester Marwa,  Aisha Juma, Zainabu Mohammed/ Sara Joel, Dotto Evarist/ Diana William,Christer John na Vioeth Mwamakamba.


Kikosi cha Burundi: Amissa Inarukundo, Chancelline Akimana, Emelyne Irankunda,  Evelyne Akimana, Neema Nzohabonayo,  Estella Gakima, Bora Inez, Rukiya Bizimana, Yasin Edgaridy,  Adolphine Salum na Joella Akimana. 


Tanzania itashuka dimbani Alhamisi ya wiki hii dhidi ya katika viwanja hivyo hivyo vya Azam Complex.

No comments:

Post a Comment

Pages