HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 25, 2023

DC TEMEKE MATINYI AMWAKILISHA RC CHALAMILA KUMPOKEA WAZIRI MKUU WA BURUNDI GERVAIS NDIRAKUBUCA


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Matinyi amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila katika mapokezi ya Waziri Mkuu wa Burundi, Gervais Ndirakobuca, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Viongozi wa nchi za Afrika wanakusanyika Jijini Dar es Salaam kuhudhuria Mkutano  wa Afrika wa Rasilimali Watu unaofanyika  kwa siku mbili tarehe 25-26 Julai, 2023.


Mwenyeji wa mkutano huo ni Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment

Pages