Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Tanzania Bara Abdlrahamn Kinana Akizungumza katika
mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Dk. Ashatu
Kijaji kwa lengo la kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM
katika kipindi cha miaka miwili na nusu chini ya uongozi wa Rais Dk.
Samia. (Picha zote na Fahadi Siraji CCM)
Makamu mwenyekiti Abdlrahamin Kinana
akipeana mkono na makatibu wa Kata wa CCMM mara baada ya kukabidhi
pikipiki 21 zilizonunuliwa na Mbunge wa Kondoa Vijijini Dkt Ashatu
Kijaji katika mkutano wa hadhara
ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Dk. Ashatu Kijaji kwa lengo la
kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika kipindi cha
miaka miwili na nusu chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia.Na Mwandishi Wetu, Kondoa
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahaman
Kinana, amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa
ndani ya kipindi cha miaka miwili kutokana na uongozi wake mzuri
unatokana utulivu, usikivu, kupokea ushauri na kufanya uamuzi wa busara
kwa manufaa ya Watanzania.
Kinana
ameyasema hayo jana wilayani Kondoa mkoani Dodoma katika mkutano wa
hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Dk. Ashatu Kijaji kwa
lengo la kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika kipindi
cha miaka miwili na nusu chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia.
“Kwa
hali ilivyo na kwa hatua tuliyopiga tukienda hivi tunavyokwenda mpaka
kufika 2025 mimi nina uhakika kila Mtanzania atakuwa na sababu ya kusema
tuendelee na CCM, tuendelee na Rais Samia Suluhu Hassan. Hatutokuwa na
sababu nyingine yoyote kwanza ni utamaduni wetu Chama Cha Mapinduzi
hatubadilishi uongozi katikati ya safari, ukitaka kubadilisha sababu
itakuwa nini, hakuna.
“Lazima
tumpe mtu nafasi yale aliyokusudia chini ya uongozi wa Chama chetu
yatimie, ikifika 2025 tunakwenda na Rais Samia na Mwenyekiti wetu wa
Mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa amesema kila eneo, kila kata, kila mtaa kila
jimbo yako ya kusemea mema, hatuahidi miujiza lakini tumeahidi na yale
tuliyoahidi tumeyatekeleza kwa ufanisi mkubwa sana.
“Hatusemi
haya kwa kujivuna bali kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM lakini
tunaangalia na wenzetu wa nchi jirani wanakwendaje. Nchi yetu imetulia,
inamaani, ina umoja, inamshikamano, nchi ina malengo, na ina mipango
ambayo inatekelezwa na kila mtu ni shahidi, CCM itaendelea kuchaguliwa
kwa sababu ina sera nzuri ina Ilani nzuri inayotekelezeka,” alisema
Kinana.
Aidha,
alisema kuna watu wamejaribu kutugawa kwa misingi ya udini wameshindwa,
kuna watu wamejaribu kutugawa kwa misingi ya ukabila wameshindwa, kuna
watu wamejaribu kutugawa kwa misingi ya ubara na visiwani wameshindwa
huku akifafanua katika Bara la Afrika ziko nchi nyingi zimeajaribu
kuungana na wanazifahamu ikiwemo Afrika Magharibi na nchi za Uarabuni
zote zimesambaratika umoja haupo, lakini Tanzania muungano wao
umeendelea kuwa imara na mwakani muungano huo unafikisha miaka 60.
“Sababu
ni misingi imara iliyojengwa na wasisi wa taifa letu hayati baba wa
Taifa Mwalimu Julius Nyerere na marehemu Abeid Aman Karume, misingi
yenyewe migumu na mnakumbuka katika kipindi mbalimbali muungano wetu
umepitia kashikashi lakini tumeendelea kuwa imara,” alisema.
Pamoja
na hayo Kinana alisema anaungana na wananchi wote pamoja na viongozi
kumpongeza Mwenyekiti wa Chama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. Samia kwa uongozi wake madhubuti. “Wakati mwingine baadhi
ya watu wanaona kama vile labda tunamsifu sana ndugu Rais lakini
hatumsifu kwa mambo ambayo hayana uhakika, kama nilivyosema ushahidi
upo.”
“Baadhi
yenu mlifuatilia Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Dodoma mwezi wa 12
taarifa ilitolewa pale ikaelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi ya miaka miwili na miaka miwili hiyo wakati huo ilikuwa ni ya
Rais Samia. Amefanya kazi kubwa sana na ili muweze kutekeleza kazi zenu
vizuri lazima muwe na fedha za kutosha.
“Fedha
hizo ni mapato ya ndani, mapato ya nje. Mapato ya ndani ya makusanyo
yaliyokusanywa na serikali na taasisi zake mbalimbali miaka hii miwili
kwa kila mwezi yako juu kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi
yetu, makusanyo yamefanikiwa bila mtu kusukumwa, bila kutishwa bila mtu
kuwekwa mahabusu.
“Mapato
kutoka nje yamekuja kwa sababu Rais na serikali yake chini ya uongozi
wa Chama Cha Mapinduzi wamejenga mahusiano mazuri sana, dunia leo
inatuamini zaidi, inatuheshimu zaidi, inatuthamini zaidi, nchi
inakopesheka kuliko wakati wowote. Hivi karibuni kulikuwa na mashirika
mawili duniani ambayo yanafanya tathimini ya hali ya uchumi na namna
nchi inavyoweza kukopesheka.
“Mashirika
yote mawili yametoa alama ya juu sana kwa serikali ya Chama Cha
Mapinduzi inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, maana yake ni nini
ukitaka kupewa msaada hawa wanaaminika, watatumia misaada vizuri
hawataiba, hawatatumia vibaya, hatawapoteza mkitaka kwenda kutafuta
mkopo kwa tathimini yao Tanzania tunakopesheka,” alisema.
Awali
akielezea utekelezaji wa Ilani katika Jimbo la Kondoa Vijijini Dk.
Kijaji alimpongeza Rais Samia kwa kuitazama kwa karibu Kondoa ambapo
katika kipindi cha miaka miwili na nusu miradi ya maendeleo imepelekwa
katika sekta mbalimbali na hiyo ni kutekeleza ahadi ya Chama Cha
Mapinduzi kupitia Ilani yake ya Uchaguzi.
“Kwa
kipekee nimshukuru Serikali ya CCM ya Awamu ya Sita chini ya uongozi
thabiti wa Dk.Samia kwa kutekeleza kwa vitendo na kwa ufanisi mkubwa
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 .Kwa wananchi wetu wa Jimbo la
Kondoa kila mmoja wetu anaona kwa macho miradi mingi ya maendeleo
inayotekelezwa katika vijiji na vitongoji ,hivyo basi naomba muendelee
kukiamini Chama Cha Mapinduzi.”
Wakati
wabunge na Wajumbe wa Halmashauri ya Taifa(NEC) ambao wamepata nafasi
ya kuzungumza katika mkutano huo wameeleza kwa kina hatua ambazo
zinachukuliwa na Serikali katika kuboresha sekta ya bandari nchini huku
wakitoa rai kwa wananchi kutosikiliza maneno ya upotoshaji yanayotolewa
na baadhi ya watu ambao kimsingi wameishiwa hoja.
No comments:
Post a Comment