HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 23, 2023

MAONESHO YA 18 YA ELIMU YA JUU SAYANSI NA TEKNOLOJIA YAFIKA MWISHO

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga, akitoa hotuba yake wakati wa kufunga maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazo Mmoja jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, akitoa hotuba yake wakati wa kufunga Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipang (katikati), akpata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uratibu wa Udahili na Menejimenti ya Data Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Dk. Kokuberwa Katunzi (kushoto) alipotembelea banda la TCU wakati wa kufunga Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa.

 

Naibu Waziri wa Elimu, Omary Kipanga (kushoto) akimkadhi cheti Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, wakati wa kilele cha Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga (kushoto), akimkadhi cheti Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi inayosaidia wanafunzi kusoma nje ya nchi (Universities Abroad Representative), Tony Kabetha, wakati wa kufunga Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Mipango Utawala na Fedha, Prof. Allen Mushi (kushoto) akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa chuo hicho wakati wa kilele cha Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
 Washiriki na wawakilishi wa vyuo vya elimu ya juu kutoka nje ya nchi wakiwa katika picha ya kumbukumbu.

 

Na John Marwa

 
MAONESHO ya 18 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia yamefika tamati huku taasisi za elimu ya juu zikiaswa kuendelea kuzingatia yale yote waliyojifunza kwa manufaa ya maendeleo ya kiuchmi na kijamii.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga, ambaye amehitimisha maonesho hayo huku akiziasa taasisi za elimu ya juu na taasisi za utafiti kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia mpango wa tatu wa Taifa wa maendeleo.

"Napongeza taasisi zote zinazoshiriki maonesho haya, kwa ubunifu na maandalizi mazuri ya ushiriki wenu kwenye maonesho haya.

"Ni rai yangu kwamba kupitia maonesho haya tunaendelea kupata fursa ya kubadilishana ujuzi na na uzoefu katika maeneo mbalimbali na kufikia malengo ya mafunzo na utoaji mafunzo kwa kuzingatia mahitaji ya jamii na Taifa letu kwa ujumla.

"Maonesho ya mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu isemayo 'Kukuza ujuzi nchini kupitia elimu ya juu sayansi na teknolojia kwa uchumi imara na shidani' mtakubaliana nami kwamba hivi sasa tunaishi kwenye Ulimwengu wenye ushindani mkubwa, sio tu kiuchmi na kijamii."amesema .....na kuongeza kuwa.

"Lakini kutokana na maendeleo makubwa na haraka ya Sayansi na Teknolojia kila siku tunashuhudia ubunifu wa teknolojia mpya na ubunifu wa ufumbuzi wa mambo mbalimbali yenye lengo la kuboresha na  kurahisisha maisha.

"Hivyo kauli mbiu hii inatoa changamoto kwetu sote na hususani taasisi zinazoshiriki maonesho haya kujipambanua na kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu hii.

"Taasisi zetu za Elimu ya Juu zina mchango mkubwa katika kuleta mageuzi makubwa ya kiuchmi kwa kuhakikisha wana uchumi wetu wanapata ujuzi na maarifa stahiki na shindani katika soko la ajira na wanashiriki kikamilifu kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchmi na kustahimili ushindani kitaifa, kikanda na kimataifa." Amesema.

"Kabla sijahitimisha hotuba yangu, napenda kusisitiza umuhimu wa Taasisi zetu za Elimu ya Juu kujikita katika matumizi ya sayansi teknolojia na ubunifu ili kutimiza adhma ya Serikali kama ilivyoainishwa katika mpango wa tatu wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano 2021/2022 hadi 2025/2026.

"Mpango huu pamoja na mambo mengine unasisitiza na kuhimiza matumizi ya sayansi teknolojia na ubunifu, matumizi ya takwimu, mitambo inayojiendesha, kampyuta na roboti.

"Ninaamini kwamba taasisi za elimu ya juu na taasisi za utafiti na  maendeleo ambazo kwa sehemu kubwa ndio washiriki wa maonesho haya, ndio wadau muhimu na sahihi na kutekeleza na kutimiza adhma ya  mpango huu wa tatu wa maendeleo ya taifa katika eneo hili la matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu kama nyenzo muhimu ya kuchochea uzalishaji na kukuza uchumi wa nchi." Amesisitiza kwa kutoa rai kuwa.


"Hivyo, natoa rai kwa taasisi zote za elimu ya juu na taasisi za utafiti na maendeleo kuchangamkia fursa hii kwa kuelekeza taasisi na bunifu zake katika maendeleo yaliyoainishwa kwenye mpango wa tatu wa Taifa wa maendeleo ya miaka mitano.

"Kwa upande wetu kama Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia tumeendele kuwatambua, kuwaendeleza wabunifu nchini kwa lengo la kuchangia maendeleo ya kiuchmi na kijamii.

"Wizara ilitoa mafunzo kwa wabunifu wachanga 83 na kutoa rasilimali fedha kwa wabunifu 27 wlioenguliwa katika mashindano ya kitaifa ya sayansi teknolojia na ubunifu. Kwa lengo la kuendeleza bunifu na teknolojia zao ili kufikia hatua ya ubunifu."

"Leo hii tunahitimisha maonesho haya tunakila sababu ya kujivunia mafanikio makubwa katika sekta ya elimu kwa ngazi zote za elimu na mafunzo nchini. Itoshe tu kusema kila mwenye macho haambiwi tazama na kila mwenye masikio asikie haya tunayoyazungumza jinsi ambavyo sote tunavyoshuhudia kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita, chini ya uongozi thabiti wa Mama yetu Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Ninafahamu kwamba Julai 15 mwaka huu TCU ilitangaza kufunguliwa kwa dirisha la udahili kwa waombaji wa Shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 23/24, nimejulishwa kwamba  waombaji wengi wametumia fursa zinazofanywa hii ya maonesho kuomba udahili wa vyuo na programu mbalimbali za masomo wanazozipenda.

"Napenda nitumie fursa hii kutoa rai kwa menejimenti za vyuo vyote vilivyo ruhusiwa kudahili wanafunzi kwa mwaka huu kuhakikisha wanasimamia ipasavyo zoezi hili la udahili kuepuka changamoto na usumbufu usio kuwa wa lazima kwa waombaji, wazazi, walezi na taasisi za udhibiti ubora na Serikali kwa ujumla." Amesema.


No comments:

Post a Comment

Pages