HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 29, 2023

MCHAWI MWEUSI AZIVUTIA KASI ZANZIBAR, UGANDA CECAFA U18

Na John Marwa

KOCHA Mkuu wa timu ya Tanzania ya wasichana U-18, Bakari Shime 'Mchawi Maeusi' amesema bado anakibarua kigumu dhidi ya Zanzibar na Uganda katika mashindano ya kuwania ubungwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA U18).

Tanzania ni wenyeji wa mashindano hayo, ambapo wamefanya vizuri katika michezo miwili dhidi ya Burundi katika mchezo wa ufunguzi na juzi walicheza na Ethiopia ambao wamekubali kichapo cha mabao (2-0), katika uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumza na Habari Mseto Blog amesema, anawapongeza wachezaji wake kwa kupambana na kufuata maelekezo yaliyo pelekea kupata ushundi huo katika michezo miwili ya awali.

Amesema baada ya kupata ushundi mnono dhidi ya Ethiopia, kipindi cha kwanza walifanikiwa kucheza vizuri kwa wachezaji wake kufanikiwa kufanya kile alichowafundisha mazoezi na kuhamishia katika mechi.

“Kipindi  cha pili kilikuwa kigumu kwetu kwa sababu ya umakini wa Ethiopia, lakini tumelinda bao na kuongeza bao ligine, kazi kubwa ilikuwa ni kutengeneza nafasi, mechi ya kwanza na Burundi  tulitengeneza nafasi japo hazikuwa bora.

"Mechi  hii tumeweza kutengeneza mashambulizi yaliyo bora na kufanikuwa kushinda mabao 2-0 na katika michezo miwili jumla tumefunga mabao 5, ni jambo la kuwapongeza sana vijana wangu,” amesema Shime.

Ameongeza kuwa waliwanyima nafasi Ethiopia ya kufanya mashambulizi kwa kuwazuia kwenye njia zao, kwani haikuwa mechi rahisi kwao na watahakikisha wanafanikiwa kujipanga zaidi na mechi mbili zijazo.

“Mechi dhidi ya Zanzibar sio rahisi, tunahitaji kupambana kushinda mechi hiyo baada ya hapo tunaenda kupanga jinsi ya kumalizia hatua hii dhidi ya Uganda, katika  mashindano haya, niliofia sana timu ya Ethiopia lakini umeona tumefanikiwa kupata matokeo ,” amesema Shime.

Shime amebainisha kuwa hakuna mechi rahisi,  haichukulii Zanzibar ni timu rahisi sana kwa sababu mechi ya kwanza walisumbuliwa na  Burundi na hatimaye kupata matokeo katika kupindi cha pili.


Kuhusu kutwaa ubingwa wa mashindano hayo, Shime, amesema malengo yao ni kuona wanabakiza kombe hilo katika ardhi ya Tanzania na kupambana katika kila mechi kupata ushundi ili kufikia kinachotarajiwa na watanzania kutoka kwa wasichana hao.



No comments:

Post a Comment

Pages