HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 29, 2023

YANICK BANGALA ATUA AZAM FC

Na John Marwa


Kiungo wa kazi raia wa DR Congo na Klabu ya Yanga Yanick Bangala ametua kwa waoka mikate wa Chamazi wa Azam FC kwa kandarasi ya miaka miwili.


Bangala ametua mitaa ya Chamazi Complex mchana wa leo kwa kutambulishwa na uongozi wa Klabu hiyo mara baada ya fununu za muda mrefu kutokuwa sehemu ya kikosi cha Yanga SC.


Azam wamekamilisha  dili hilo ikiwa ni kuimarisha kikosi chao huku akiwa mchezaji wa pili kutoka Yanga kujiunga na Azam FC dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi.


Ikumbukwe kuwa Bangala ameitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa katika misimu miwili iliyopita akifanikiwa kuipatia Yanga mataji mawili ya Ligi, mawili ya Azam Sports Federation Cup, na Ngao ya jamii huku akiifikisha hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC.


Bangala pia alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa Ligi 2021/2022. 



Kusajiliwa kwake Azam niwazi kuna mchezaji mmoja ndani ya Azam ataonyeshwa Mlango wa kutokea kwa wachezaji wa kimataifa kwani kabla ya usajili wake idadi ilishatimia ya wachezaji 12.

No comments:

Post a Comment

Pages