HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2023

'Mtu yeyote anaweza kulima Mkonge'



Afisa Masoko na Uhamasishaji wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), David Maghali akiwahudumia wateja katika Banda la TSB lililopo kwenye Viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya 47 ya Biashara Dar es Salaam maarufu Sabasaba.

Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Esther Mbusi, akizungumza na wateja waliofika katika Banda la TSB lililopo katika Maonesho ya Kimataifa ya 47 Biashara Dar es Salaam maarufu Sabasaba lililopo katika Ukumbi wa Katavi (Katavi Hall) mkabala na Banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona (kushoto) akitoa maelekezo kwa Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Bodi hiyo, Esther Mbusi katika Banda la TSB lililopo kwenye Viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya 47 ya Biashara Dar es Salaam maarufu Sabasaba.

 

Na Irene Mark

BODI ya Mkonge Tanzania (TSB), imewatoa hofu watanzania wanaotaka kujikita kwenye kilimo cha zao la Mkonge kuhusu fursa mbalimbali ikiwamo masoko.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhamasishaji wa Bodi, David Maghali amesema hayo alipokuwa akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wadau mbalimbali waliotembelea katika Banda la TSB kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam maarufu Sabasaba leo Jumamosi Julai 8.

Wadau hao walitaka kujua kama mtu mmoja mmoja au mkulima mdogo anawezaje kujikita kwenye kilimo hicho na fursa za masoko.

Amesema  miongoni mwa masuala wanayotoa elimu katika banda hilo ni kuhusu masoko, fursa na sekta nzima kwa ujumla huku akisisitiza kuwa mwananchi yeyote anaweza kulima Mkonge.

"Mtu yeyote anaweza kulima Mkonge kwa usaidizi wa Bodi tunaweza kumpa ushauri wa kilimo bora na kumuunganisha na masoko, soko la Mkonge lipo na ni la uhakika ndani na nje ya nchi.

"Mahitaji ya Mkonge kwa sasa ni makubwa kutokana na fursa zake na bidhaa zinazozalishwa kutokana na zao hilo lakini lakini pia  kufanya tafiti mbalimbali," amesema.

Watu wamejitokeza katika Banda hilo la TSB lililopo katika Ukumbi wa Katavi (Katavi Hall) mkabala na Banda la Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kupata elimu na kujifunza Kilimo cha Mkonge na fursa mbalimbali zinazotokana na zao hilo na sekta nzima kwa ujumla.




No comments:

Post a Comment

Pages