HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2023

Muharami Mchume kukabidhiwa tuzo ya Pierre de Coubetin Desemba


Na Mwandishi Wetu


MWANAMICHEZO mahiri hapa nchini, Muharami Mchume Desemba mwaka huu anatarajiwa kukabidhiwa tuzo ya mwanzilishi wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), Pierre de Coubetin atakayokabidhiwa jijini Younde, Cameroon.


Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Pierre de Coubetin (IPCC), Dk Evele Melisa Atour hatua hiyo imetokana na kikao cha bodi kilichoketi Juni 25 mwaka huu kilichojadili masuala mbalimbali yakiwemo maendeleo ya kiuvumbuzi kama aliyoyatekeleza Mchume.


Atour alisema kwa aliyoyatekeleza Mchume ni sehemu yake ya pongezi kwa aliyoyatekeleza kwa maendeleo ya michezo duniani.


Awali, Januari 28 mwaka huu, Mchume aliteuliwa katika Kamati ya IPCC akiwa ni mjumbe aliyepitishwa na Mkutano Mkuu uliofanyika jijini Lausanne Uswisi.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa IPCC,  Stephan Wassong wakimteua Mchume baada ya kusambaza falsafa za mwanzilishi wa IOC, Pierre de Coubetin na kuipa thamani kamati hiyo duniani.


Uteuzi wa Mchume umetokana na ombi la kukitafsiri kitabu cha historia ya mwanzilishi huyo kwa lugha ya Kiswahili.


Pierre de Coubetin alizaliwa Januari mosi, 1863 na alifariki Septemba 2, 1937.


Akizungumza baada ya kupata barua hiyo ya mwaliko wa tuzo, Mchume alisema hatua hiyo ni heshima kwa Tanzania kwani aliyoyatekekeleza yanaitangaza nchi nje ya mipaka.




Mchume alisema pia tuzo hiyo atakayokabidhiwa Cameroon ataiwasilisha Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

No comments:

Post a Comment

Pages