Afisa
Udahili Chuo Kikuu Mzumbe, Nringi Urassa, akitoa maelezo kwa wanafunzi
waliotembelea banda la Chuo hicho kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya
Kimataifa (Sabasaba) Julai 1, 2023.
Kaimu
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa
Kitaalam( DVC ARC) Dkt. Eliza Mwakasangula(kulia) akiangalia Moja wapo
ya bidhaa zilizotengenezwa na Mercy Mwambe , Mwanafunzi wa Masomo ya
Shahada ya Uongozi wa Biashara katika Ujasiliamali na Ubunifu (BBA EIM).Mhitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe 2022, Aron Msonga, akichangia fedha kwa ajili ya Ujenzi Hosteli ya Wanafunzi wa Kike Ndaki ya Mbeya, alipotembelea Banda la Chuo hicho kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kimataifaji na Baraza la Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Lucy Massoi.
Mkurugenzi wa Kimataifaji na Baraza la
Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Lucy Massoi (kushoto) akionesha muhamala aliochangia mhitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Martine Thomas, kwa ajili ya Ujenzi
Hosteli ya Wanafunzi wa Kike Ndaki ya Mbeya, alipotembelea Banda la
Chuo hicho kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)
jijini Dar es Salaam.
Na Tatu Mohamed, Dar es Salaam
KAIMU
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe anaeshughulikia taaluma,
utafiti na ushauri, Dk. Eliza Mwakasangula amewakaribisha Watanzania
wote kutembelea banda lao lililopo katika Maonesho ya Biashara ya 47 ya
Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
katika viwanja hivyo amesema katika huduma mbalimbali ambazo zinatolewa
katika chuo hicho hivyo wafike kuweza kujionea.
"Tunawakaribisha
watu wote kwani tunahuduma mbalimbali, tunadahili wanafunzi kwaajili ya
kujiunga na Program zetu Chuo Kikuu Mzumbe kwa ngazi ya Shahada za
awali kwa wale waliomaliza kidato cha nne, kidato cha Sita na hata
waliomaliza muda mrefu," amesema.
Amesema
Chuo Kikuu cha Mzumbe ni miongoni mwa vyuo vinavyotoa Mafunzo
mbalimbali ikiwemo masomo ya Biashara, Utawala, Sheria, Uhasibu, Sayansi
na Teknolojia ambapo wanateknolojia mbalimbali kwa vijana wao ambao
wamekuwa wakizianzisha chuoni hapo.
"Chuo
chetu kina kampasi tatu ambapo ni Mkoa wa Morogoro, Dar es Salaam
maeneo ya Upanga na Tegeta pamoja na mkoani Mbeya," amesema.
Aidha
Dk. Eliza amewaomba Watanzania wakiwemo Wanafunzi waliomaliza Chuo
hicho miaka ya nyuma (Alumni) kujitokeza na kuchangia kampeni ya ujenzi
wa bweni la wanafunzi wa kike mkoani Mbeya.
Amesema kwa kufanya hivyo ni ishara ya
kurudisha kitu kidogo kwa jamii ikiwa nao ni wanajamii wa Chuo Kikuu Mzumbe.
"Ujenzi
wa bweni hilo tayari umezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambapo
kuna namba maalum ya uchangiaji hivyo niwakaribishe wanafunzi
waliosoma Mzumbe kuweza kuchangia," amesema.
Licha
ya kuwakaribisha pia amewaomba wananchi kwa ujumla kuchangia ujenzi wa
hosteli za Wanachuo wa kike katika kampasi ya Mbeya kupitia control
namba 994180331310.
No comments:
Post a Comment