HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 01, 2023

THANK YOU YAMFIKIA SAWADOGO

 

Na John Richard Marwa 


Klabu ya Simba imetangaza kuachana na kiungo wake mkabaji Ismail Sawadogo ambaye usajili wake ulifanyika kipindi cha dirisha dogo la msimu wa 2022/23.   


Kwa mujibu wa Taarifa ya klabu ya Simba imeeleza kuwa wamefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuachana na kiungo huyo.



Awali iliripotiwa kuwa  kiungo huyo alihitaji kulipwa milioni 700 Ili kuvunjwa mkataba wake ambapo alikuwa na kandarasi ya miaka miwili ndani ya mitaa ya Msimbazi.



Ikumbukwe mechi ya kwanza kwa kiungo huyo ilikuwa ni kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Simba katika dimba la Jamhuri na kumalizika kwa Mnyama kushinda bao 0-1. Mchezo wa NBC PL 

No comments:

Post a Comment

Pages