HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 30, 2023

NI VITA YA NDUGU CECAFA U-18 LNI VITA YA NDUGU CECAFA U-18 LEO, CHAMAZI COMPLEX


Na John Marwa


TIMU ya Taifa ya Tanzania ya wasichana (U-18) inashuka dimbani leo kuvaana na ndugu zao kutoka Visiwani Zanzibar  katika mashindano ya kuwania ubingwa wa ukanda wa Afrika  Mashariki na Kati  (CECAFA).


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira y saa 12:00 ya jioni,  baada ya kukamilika kwa mchezo wa kwanza kati ya Ethiopia dhidi ya Burundi utakaopigwa saa 9:00 alasiri, ambapo michezo yote inalindima uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Tanzania ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo.


Tanzania inashuka dimbani wakitoka kupata matokeo mazuri katika michezo miwili ya awali waliyocheza kwa kuwafunga Burundi 3-0 na kushindi mabao 2-0 dhidi ya Ethiopia.


Wakati  Zanzibar, hii itakuwa mechi yao ya pili katika mashindano hayo baada ya kuanza vibaya kwa kukubalia kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Uganda. 


Katika mchezo wa leo timu zote zinahitaji matokeo kujiweka sehemu salama ya kuendelea na mashindano hayo huku Tanzania ikidhamilia kutwaa ubingwa wa CECAFA  U -18. Ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika mashindano hayo.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti makocha wa timu hizo, kocha wa Tanzania Bakari Shime alisema ni mechi ngumu, Zanzibar walionyesha kiwango kizuri katika mechi yao ya kwanza kwa kucheza vizuri kipindi cha kwanza dhidi ya Uganda.




“Hii mechi  sio rahisi, tunahitaji kupambana kushinda nina imani watakuja kivingine tofauti na walivyocheza mechi yao ya kwanza, kikubwa wachezaji wako tayari kwa ajili ya kupambana kusaka ushindi katika mechi yetu ya kesho (leo),” amesema Shime.


Amesema hakuna mechi rahisi,  haichukulii Zanzibar ni timu rahisi kwa sababu mechi ya kwanza walisumbuliwa na  Burundi na hatimaye kupata matokeo katika kupindi cha pili.


Naye  Kocha Mkuu wa Zanzibar,  Abdulmutik Haji amesema baada ya kufanyia kazi mapungufu ya mechi ya kwanza sasa wako tayari kusaka ushindi dhidi ya Tanzania.



“Tumejiandaa vizuri, wachezaji wangu wako tayari kwa mchezo huo, nina imani utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani kwa sababu tunahitaji kupata matokeo chanya dhidi ya Tanzania,” amesema Abdulmutik.

No comments:

Post a Comment

Pages