HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 31, 2023

MWENYEKITI HALMASHAURI YA MJI KIBAHA AMUOMBA RAIS SAMIA KUPANDISHA HADHI KIBAHA KUWA MANISPAA

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Mussa Ndomba  akisoma waraka huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha,Nickson Simon, akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Kibaha (UWT) Mwalimu Mwajuma Nyamka wakati akiingia kwenye Ukumbi  wa Halmashauri ya Mji Kibaha.



Na Khadija Kalili, Kibaha

MWENYEKITI wa  Halmashauri  ya Mji Kibaha Mussa Ndomba  amemuomba  Mheshimiwa  Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan  kuipandisha hadhi Halmauri ya Mji Kibaha  na Kuwa Manispaa  kwa sawababu imekidhi sifa na vigezo kwa asilimia 78 kuwa Manispaa.

"Nasema haya kwa sababu Mkoa wa Pwani ni kati ya Mikoa mikongwe ambao umeasisiwa 1975 hivyo hata Halmashauri  ya Mji  Kibaha  ni Kongwe ambayo pia ni Makao Makuu ya Wilaya zote ndani ya Mkoa wa Pwani hivyo tunamuobma Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  atupandishe hadhi  na kuwa Manispaa  kwani jambo hili limeshazungumzwa sana  katika mikutano mbalimbali  ya Siasa  nchini kadhalika Mbunge wetu wa Jimbo la Kibaha Mjini Mheshimiwa Silyvestery  Koka amelisemea sana  akiwa katika vikao vya  Bunge Jijini Dodoma pia niwakumbushe ndugu wajumbe hata kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 jambo hili limezungumziwa kwenye majukwa ya siasa" amesema Ndomba.

Wakati huohuo Mwenyekiti  huyo amesema kuwa  kwa niaba ya Madiwani na  viongozi wa Halmashauri Kibaha anamuomba Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  kutoa idhini ya kumegewa eneo la Shirika la Elimu Kibaha kwa ukubwa wa ekari 576  lililopo kandokando ya  barabara  iendayo Morogoro  ikiwa ni katika  kuweka mandhari nzuri na ya kuvutia ya Halmashauri ya Mji  Kibaha iliyopo  Mkoani  Pwani kwa wanaoingia na kutoka.

"Mheshimiwa Rais  tunamuomba atupatie eneo la ukubwa  wa hekari 576 ili Halmashauri  iweze kuweka mipango miji mizuri ikiwemo uwekezaji kwa wafanyabiashara na kuuweka mji katika hali ya kuvutia pindi unapoingia, Kibaha ni  Wilaya mama na lango la kuingia Mji wa  mkubwa wa biashara Dar es  Salaam  tofauti na ilivyo hivi sasa  kwani  hakuna mandhari nzuri kwa sababu ya kuonekana mapori tu ambayo kwa sasa ni eneo linalomilikiwa na Shirika la  Elimu Kibaha  lenye ukubwa wa  hekari zaidi ya  3000 ambazo wahusika wameziacha zikiwa mapori   bila ya kufanya  jitihada zozote za kuendeleza katika eneo hilo"amesema Ndomba.

Amesema kuwa endapo Halmashauri  ya Mji Kibaha itapatiwa eneo hilo la ukubwa wa hekari 576 tu watapanga  shughuli  za  maendeleo  ya Mji Kibaha.

Mwenyekiti  Ndomba amesema hayo  katika kikao   cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne ya mwaka  kilichofanyika mwishoni mwa wiki  na kuhudhuriwa na viongozi  mbalimbali  kutoka vya ma vya siasa , wakuu wa Idara zote  na wataalamu  ndani ya  Halmashauri  hiyo akiwamo Mkuu wa Wilaya Kibaha Nickson Simon, Mkurugenzi Mhandisi Mshamu Ali Munde pamoja  na   wananchi wa Wilayani hapa.

No comments:

Post a Comment

Pages