HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 25, 2023

SIMBA DAY NI 'UNYAMA MWINGI '

Na John Marwa


Uongozi wa Klabu ya Simba umeweka wazi mikakati yao kuelekea tamasha kubwa la wiki ya Simba na kilele cha Simba Day ambapo lengo ni kurejesha kwenye jamiii na kuwatambulisha wachezaji wao kwa mashabiki.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Imani Kajula amesema amesema wiki ya Simba ni wiki ya 

kurudisha kwa Jamii.


"Wiki ya Simba ni wiki ya kurudi kwa jamii, wiki ya kutambulisha wachezaji wapya kwa mashabiki wetu, Simba kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji na kuchangia damu." 


"Kambi ya Uturuki inaendelea vizuri." 


"Wiki hii tunatarajia kufanya mnada wa kibegi pamoja na jezi zile na mapato yake yatasaidia ujenzi wa wodi ya kina mama na mtoto kwenye hospitali ya Muhimbili na Zanzibar." Amesema na kuongeza kuwa.


 "Niwashukuru washirika wetu wakubwa wa Simba Week na Simba Day. Mabenki yote ya CRDB na NMB watawawezesha mashabiki wa simba kufungua account za simba za kawaida, za watoto na wakinamama" 


"Wiki ya Simba tumeibatiza kuwa ni wiki ya UNYAMA MWINGI. SIMBA WEEK, UNYAMA MWINGI, SIMBA DAY, UNYAMA MWINGI. Unyama Mwingi inawasilisha mambo mengi ambayo yatatokea ndani ya wiki hii." - CEO Imani Kajula.

No comments:

Post a Comment

Pages