HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 25, 2023

POWER DYNAMOS KUNOGESHA SIMBA DAY

Na John Marwa


KLABU ya Simba SC imetangaza kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na Mabingwa wa Zambia Power Dynamos katika kilele cha wiki ya Simba Day Agosti 6, 2023.


Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kuelezea matukio ya wiki ya Simba leo jijini Dar es Salaam Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba Ahmed Ally amesema watacheza na Mabingwa wa Zambia Power Dynamos.

"Katika kilele cha wiki ya Simba tutacheza na Bingwa kutoka nchini Zambia Power Dynamos, tunawalete Mabingwa wa Zambia ambao pia watakuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL kama sisi.


" Sambamba na hilo upande wa Burudani tutakuwa na wasanii wa ndani na kimataifa. Wandani wataongozwa na watoto wa nyumbani ambapo Kaptain Tundaman atawaongoza na wengine tutaendelea kuwatambulisha mmoja mmoja" amesema All nankuweka wazi viingilio vya Simba Day Unyama Mwingi.


"Tumeamua kuweka Viingilio rafiki kwa sababu Simba Day ni tamasha la wanasimba sio sehemu ya kwenda kutafuta mapato bali kuwakutanisha wanasimba kuja kuona wachezaji wao.


"Viingilio vya Simba Day Mzunguko 5000

Machungwa, 10,000, VIP C, 20,000, VIP B, 30,000, VIP A 40,000 huku 

Platinum TSH  200,000.


"Ambapo nusu ya gharama katika tiketi ya Platinum zitakwenda kwenye ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika hospital ya Taifa ya Muhimbili na Mnazi mmoja Zanzibar" amesema Ahmed Ally.

No comments:

Post a Comment

Pages