HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 25, 2023

SIMBA MTEGONI KWA POWER DYNAMOS

Na John Marwa


WAKATI Klabu ya Simba ikitangaza kucheza na Mabingwa wa Zambia Power Dynamos katika kilele cha wiki ya Simba 'Simba Day 2023' 



Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF limetangaza ratiba ya hatua za awali na hatua za kwanza za mashindano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.


Ratiba hiyo ni kama mtego kwa Lunyasi na wageni wao hao kutoka Zambia Power Dynamos ambapo Power Dynamos katika hatua za awali watacheza na African Stars na mshindi baina yao atakutana na Simba hatua za awali.


Kama Power Dynamos watafanikiwa kuwaondosha African Stars watakutana tena na Simba ambao ni wenyeji wao katika tamasha lao la wiki ya Simba 'Unyama Mwingi'.


Lakini pia kama African Stars watawaondosha Power Dynamos basi watakutana na Mnyama Simba katika hatua ya awali na mshindi wa jumla atatinga hatua ya makudi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL.

No comments:

Post a Comment

Pages