HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 25, 2023

CAF YAITUPA YANGA DJIBOUTI CAF CL

Na John Marwa

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika CAF limetangaza ratiba ya hatua za awali mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL ambapo Mabingwa wa Tanzania Yanga SC wataanzia hatua za awali dhidi ya Asas ya  Djibouti.


Mchezo wa kwanza utapigwa nchini Djibouti kisha kurejeana hapa nchini.


Mshindi wa jumla katika michezo hiyo miwili atakutana na mshindi kati ya AS Otoho ya Congo dhidi ya El Merreikh ya Sudan. Na mshindi wa jumla atatinga hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL.

No comments:

Post a Comment

Pages