HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 14, 2023

SIMBA SC YAIPIGA KO YANGA SC KWA NGOMA

Na John Marwa


KLABU ya Simba imemsajili Kiungo wa Dimba la kati Mcongomani Fabrice Luamba Ngoma kwa mkataba wa miaka miwili.


Ngoma anajiunga na Simba akitokea Al Hilal ya Sudan, ambako amevunja mkataba wake mara baada ya machafuko ya kivita yanayoendelea nchini humo.



Kiungo huyo ni mtawala wa dimba la kati akiwa na uwezo wa kutumika kama kiungo wa ulinzi, kiungo mchezeshaji.


Ni usajlli ambao ulisumbuliwa kwa hamu sana na Wana Lunyasi kutokana na mahitaji ya mchezaji aina ya Ngoma katika eneo lao la kiungo cha ulinzi.


Awali Ngoma alitajwa kutua Yanga SC lakini Simba waliingilia dili hilo kwa kumyakua Ngoma na leo ametambulishwa.


Ngoma pamoja na wachezaji waliopo nchini wataondoka Julai 17 kuelekea nchini Uturuki kuungana na kambi ya timu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages