Na Mwandishi Wetu (Mtandao)
Klabu ya Simba leo imecheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Turan ya ligi kuu Azerbaijan kwenye mfululizo wa Pre Season mchezo wa kwanza ilishinda 2-0, mchezo wa pili ikafungwa 1-0
Aina ya magoli waliyofunga Simba, yote yametokana na staili ya uchezaji ya Robertinho, kuzuia kwa shinikizo kubwa (high pressure style of defending) na kushambulia kwa haraka (direct style of attack)
Elewa misamiati 5 ya mpira wa miguu kupitia video za magoli ya Simba;
1. HIGH-PRESSING - Goli la kwanza la Simba limetokana na msamiati huu ambao una maana ya timu inayozuia kuanza kuzuia kwa shinikizo kubwa kwa wapinzani kuanzia kwenye theluthi ya kwanza ya wapinzani pale wanapojenga shambulizi kuanzia nyuma (build up phase), ambapo kwenye video;
Mshambuliaji wa kati wa Simba, Bocco alivyoenda kum-press beki wa Turan aliyekua na mpira
- Nyuma yake kulikua na mstari wenye watu wanne kila mmoja dhidi ya mpinzani, Baleke na Kapama dhidi ya viungo wawili wa kati wa Turan, Kibu na Modi dhidi ya mabeki wa pembeni wa Turan
2. PRESSING TRAP, huu ni mtego wanaotega wachezaji wa timu inayozuia kwa wachezaji wa timu inayoshambulia
Kitendo kilichowezesha Kibu kupokonya mpira ni Baleke kusogea mbele zaidi kumtega kipa wa Turan kutompa mpira beki wa kati na kumpa mpira kiungo ambaye yeye amemuacha free
- kusogea kwake mbele kukamshawishi kipa kupeleka mpira kwa kiungo huyo ambaye tayari alikua kwenye mtego wa Simba aliotega Baleke
3. PRESSING TRIGGER, baada ya mtego kutegwa na mpinzani kuingia kwenye mtego, tukio linalofuata ni mchezaji aliyepewa mpira kuwa under pressure (Trigger)
Kibu aliacha kumzuia beki wa pembeni na kumsogelea kiungo huyo na kumpora mpira
4. COUNTER-PRESSING, ni kitendo cha timu kuanza kuzuia pale tu inapopoteza mpira kwenye eneo lolote la uwanja kwa shinikizo kubwa, mfano ni bao la pili la Simba
5.TRANSITION, ni kitendo cha timu moja kupora umiliki wa mpira kutoka kwa timu nyingine, kitendo hichi hufuatiwa na matendo mawili
Timu iliyopora mpira kushambulia kwa haraka kabla wanaozuia kurudi kwenye shape (Counter attack)
- Wanaozuia kuzuia kwa shinikizo kubwa (Counter Pressing)
July 28, 2023
Home
Unlabelled
SIMBA SC YAONYESHANA MAKALI NA TURAN FKC, UTURUKI
SIMBA SC YAONYESHANA MAKALI NA TURAN FKC, UTURUKI
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment