HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 28, 2023

TANZANIA U18 YAENDELEA KUUWASHA MOTO CECAFA

Na John Marwa

Timu ya Taifa ya Wasichana U18 imeendelea kuuwasha moto katika mashindano ya CECAFA U18 baada ya kuishushia kipigo Ethiopia cha mabao (2-0) katika Dimba la Azam Complex.

Ulikuwa mchezo mkali kwa pande zote mbili kushambulia kwa mapigo na kutandaza Soka safi la pasi na kasi, Tanzania walilazimika kuweka presha kwenye mpira ili kuwanyima Ethiopia uhuru wa kucheza aina yao ya mpira wa pasi fupi fupi kwa kasi kubwa.

Mabao ya Tanzania yalipatikana katika vipindi vyote viwiili licha ya upinzani mkali walioupata kutoka kwa Ethiopia.

Ushindi huo unakuwa wa pili mtawalia kwa Tanzania mara baada ya kushinda mchezo wa kwanza wa mashindano hayo dhidi ya Timu ya Taifa ya Burudani U18.

Wakati kwa Ethiopia U18 licha ya kuwa timu inayocheza soka safi na la kuvutia, wameendelea kukosa bahati ya kupata matokeo ya ushindi wakipoteza mechi mbili mfululizo pamoja na mchezo wa kwanza wa mashindano dhidi ya Uganda U18 kwa bao (0-1).

Mashindano hayo yataendelea kesho kutwa jumapili ya Julai 30 kwa michezo miwili kupigwa ambapo mchezo wa kwanza utazikutanisha Uganda U18 dhidi ya Burundi U18, ukifuatiwa na Tanzania U18 dhidi ya Zanzibar U18.



No comments:

Post a Comment

Pages