HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 27, 2023

TANZANIA USO KWA USO NA ETHIOPIA CECAFA U18

Na John Marwa


Timu ya Taifa ya Tanzania Wasichana U18 leo wanashuka dimbani katika mchezo wa pili wa mashindano ya CECAFA U18 kumenyana na Ethiopia katika Dimba la Azam Complex.

Tanzania inashuka kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wa kwanza kwa mabao (0-3) dhidi ya Burundi.

Wakati Ethiopia wao walipoteza mchezo wa kwanza kwa bao (0-1) dhidi ya Uganda.

Mchezo huo utapigwa majira ya saa 18:00 kwa saa za Afrika Mashariki baada ya mchezo wa kwanza kumalizika.

Mchezo wa awali utazikutanisha Timu ya Taifa ya Zanzibar watashuka dimbani kucheza mechi yao ya kwanza ya mashindano dhidi ya Uganda majira ya saa 15:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

Uganda ambao mchezo wa kwanza waliondoka na ushindi wa bao (1-0) dhidi ya Ethiopia.


No comments:

Post a Comment

Pages