HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 27, 2023

TIPER KUTOA GAWIO LA BILIONI 2 .5 KWA SERIKALI

 

Na Magrethy Katengu


Serikali imepokea Gawio la Shilingi bilion 2.5 kutoka kampuni ya Uhifadhi mafutaTanzania International Petroleum Reserves(TIPER)  ambapo fedha hizo zitakwenda kutekeleza miradi mbalimbali nchini.

Akizungumza leo Jijini Dar es  salaam katika hafla fupi ya makabidhiano ya  kupokea gawio hilo Msajili wa hazina Nehemia Mchechu amesema lengo la huo uwekezaji ni kuona hayo makampuni yakiongezeka katika mchango wa taifa siyo ya kikodi bali kama ilivyofanya kampuni ya TIPER kutoa gawio la bilion 2.5 ikiwa tayari imeshatoa kodi yote zote serikali  


Mchechu amesema kuwa kuna baadhi ya Makampuni ambapo yatafutwa kutokana na kupitwa na wakati au huduma zake na mengine yatakwenda kuunganishwa kutokana na shughuli zake kushabiina kwani zikiunganishwa na kufanya kazi kwa pamoja italeta tija zaidi  


"kuna timu inaendelea kufanya uchambuzi zaidi na mwezi wa nane mwaka huu ripoti itapelekwa na hapo itatangazwa ni Makampuni gani yataunganishwa au kufutwa kwani wakati mwingine Kampuni imekuwa ikifanya vibaya sababu kubwa ikiwa  ni uongozi hivyo lazima wapewe muda kwa kuwavumilia hivyo na kuangalia uongozi wao  . 



Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uhifadhi Mafuta TIPER Mohamed Seif Mohamed amesema sekta ya mafuta muhimu na ni nyeti sana katika maendeleo ya nchi yeyote Duniani  ina  mchango kwa katika ukuaji wa uchumi kwani inasaidia katika usafirishaji, kilimo, pia hutumiaka kila mahali kwa aina yake 


"Sisi kama TIPER tumejipanga kuwekeza siyo tu kuhifadhi katika utunzaji wa mafuta nchini pia tumewekeza katika miundombinu mbalimbali ikiwemo mabomba,pampu za kusumia mafuta, mifumo ya umeme,teknolojia,na raslimali watu hivyo tuna mchango mkubwa katika jamii" amesema Mohamed


Hata hivyo amesema uwekezaji umekuwa ukifanyika kipindi cha miaka kumi iliyopita na zaidi na tunaendelea kwani ni jambo endelevu na tumekuwa tukifanya kwa awamu 


Pia amesema wana mafuta ambayo mengine yameshalipiwa ikiwemo ya waagizaji na baadhi ya mafuta yanasubiri kulipiwa ili yatolewe hivyo niwahakikishie wateja wetu tupo vizuri katika uhifadhi mafuta. 

No comments:

Post a Comment

Pages