HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 15, 2023

TCU YATANGAZA KUFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI KWA WAOMBAJI WA SHAHADA YA KWANZA KUANZIA KWA MWAKA WA MASOMO 2023/2024

 

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Prof. Charles Kihampa, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kufunguliwa kwa dirisha la udahili kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza kuanzia kwa mwaka wa masomo 2023



Na Mwandishi Wetu 
 

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua dirisha la maombi ya udahili kwa waombaji wa shahada ya kwanza wa mwaka wa masomo 2023/2024 kuanzia leo Julai 15, 2023 huku ikianisha sifa zinazohitajika kwa wanafunzi kusoma katika vyuo vikuu mbali mbali nchini.

Katibu Mtendaji wa TCU, Prof.Charles Kihampa amesema dirisha litakuwa wazi hadi Agosti 4, 2023 na kuwahimiza waombaji wote wa udahili kuendelea kupata taarifa sahihi kupitia tovuti ya TCU au tovuti za Vyuo mbalimbli vinavyotoa elimu ya juu.

Waombaji wote wa udahili kwa mwaka wa masomo 2023/2024 wanatakiwa kuwa na sifa stahiki za kidato cha sita, sifa stahiki za Stashahada na Cheti cha awali.

"Maombi ya udahili wa kujiunga na Shahadawa kujiunga na shahada ya kwanza utahusu waombaji waliohitimu wa kidato cha sita, wenye Stashahada (Ordinary Diploma), na wenye sifa swahili za cheti  cha awali  (Foundation Certificate) ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Ili kufahamu sifa stahiki za kujiunga na Chuo Kikuu waombaji wameelekezwa kusoma vigezo vilivyopo kwenye vitabu vya muongozo vya TCU huku pia wakitakiwa kutuma maombi yao moja kwa moja kwenye vyuo ambavyo wamevichagua na kwamba maelekezo ya jinsi ya kutuma maombi yanayotolewa na vyuo vikuu husika.

Aidha Prof. Kihampa amewapa tahadhari waombaji wote wa shahada ya kwanza ikiwa watahitaji kupata ufafanuzi wa suala lolote juu ya udahili kuwasiliana moja kwa moja na vyuo husika ama TCU.

"Tunawaasa wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu hapa nchini" amesema Prof. Kihampa.

Amesema masuala muhimu ambayo waombaji wanapaswa kuzingatia ni pamoja na kusoma muongozo wa udahili na kuuelewa, kuingia kwenye tovuti za vyuo ili kujua taratibu za kutuma maombi, kutuma maombi moja kwa moja vyuoni kupitia mifumo ya kielektoniki na kuwasiliana na vyuo ili kupata taarifa huku pia waombaji wenye vyeti vinavyoytolewa na NECTA au NACTE wakitakiwa kupata idhibati ya ulinganifu wa sifa zao kabla ya kutuma maombi ya udahili.

Aidha Tume inawakaribisha wadau wote kushiriki maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yatakayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam kuanzia Jula 17 hadi 22 mwaka huu ambapo vyuo 80 vinatarajiwa kuwepo katika maonesho hayo.


No comments:

Post a Comment

Pages