HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 07, 2023

TIRA yajipanga kufikia asilimia 50 ya Watanzania


Mwananchi akizungumza na ofisa wa TIRA kwenye banda la taasisi hiyo ndani ya viwanja vya Sabasaba.



Na Selemani Msuya


MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), imejipanga kutumia miongozo waliotoa kwa watoa huduma za bima, ili kuhakikisha ifikapo 2030 asilimia 50 ya Watanzania wananatumia bima.


Hayo yamesemwa na Meneja wa TIRA Kanda ya Mashariki, Frank Shangali wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 47 yaliyoendelea katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Shangalia amesema TIRA imeundwa kwa Sheria namba 10 ya 2009 ikiwa na majukumu ya kutoa elimu, uandikishaji na usajili wa makampuni ya bima, kulinda mteja, kuishauri serikali na mengine.


Amesema takwimu zanaonesha watu wanaopata huduma za bima ni asilimia 18, ila matarajiao yao ni ifikapo 2030 waweze kufikia asilimia 50 ya Watanzania.


Shangali amesema wanakuwa na malengo ya kufikia asilimia 50 kutokana na kasi yao ya kuchangia ongezeko la pato la taifa tangu 2019 kutoka ukuaji wa asilimia 0.58 hadi 1.68 mwaka 2021.

 
Meneja huyo amesema katika kufanikisha hayo wametoa miongozo ikiwemo kuwafanya watoa huduma watoe huduma kwa mujibu wa sheria na kanuni, kwa mfano muongozo wa ulipaji wa madai ambao unamuelekeza mtoa huduma ni nanma gani, wakati gani na njia gani atumie za kulipa madai kwa mteja.


“Muongozo huo tumetoa mwaka jana umekuwa na mafanikio makubwa, kwani tumeona wananchi wamelipwa fidia zao bila tatizo lolote na kupunguza malalamiko,” amesema.


Amesema muongozo mwingine ambao umeonesha matokeo chanya ni wa wauza bima ambao ulilenga kuongeza ajira kwa watu wenye taaluma ya bima kutumia fursa hiyo kuwafikia wananchi kila eneo la nchi.


Meneja huyo amesema muongozo mwingine ambao wametoa ni IDP ambao umejikita kwenye teknolojia kwa kutumia mitandao ya simu kutengeneza huduma za bima kupitia simu, hivyo kuondoa usumbufu wa wananchi kwenda katika maofisi.


“Muongozo mwingine ambao tumeanzisha ni ule unaofuta Sheria za Kiislam, hivyo kuwafikia wananchi wengi ambao walikuwa hawakubaliani na mfumo wa zamani,” amesema.
Amesema kupitia miongozo hiyo na Mfumo wa Usimamizi wa Biasahra za Bima za kila siku ambao unamlinda mteja iwapo atatapeliwa au bima yake haijaingia kwenye mfumo.


Shangali amesema huduma ya bima ya afya, maisha na nyumba imekuwa na mchango mkubwa ambapo kwa mwaka wanatoa zaidi ya shilingi bilioni 500 kwa wananchi.


Amesema bima ni huduma muhimu kwa maendeleo ya nchi na jamii, hivyo kutoa rai kwa Watanzania kujiunga na bima, ili kuhakikisha mali na afya zao zinakuwa salama.


Meneja huyo amesema hadi wamesajili kampuni zaidi 1,400 ambazo zinatoa huduma bima ambayo inahudumua asilimia 18 ya Watanzania kwa sasa na kwamba bado wanakaribisha wadau wengine kuwekeza katika eneo hilo kwa maendeleo ya nchi.


Amesema TIRA kwa kushirikiana na kampuni za bima wamejipanga kutoa elimu kupitia vyombo vya habari, huku wakiwataka wananchi kutumia fursa ya bima kwa wote pindi ikianza kufanya kazi.


Meneja huyo amesema TIRA inaamini sekta ya bima inaweza kuhudumia wananchi kulinda uchumi na kulinda afya yao.

No comments:

Post a Comment

Pages