HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 31, 2023

UTT AMIS yajivunia mafanikio ya Utendaji Kazi


 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya UTT AMIS, Simon Migangala, akizungumza na Wahariri wa Vyomba mbalimbali vya Habari kuhusu mafanikio ya utendaji kazi wa taasisi hiyo. Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya UTT AMIS, Daudi Mbaga, akifafanua jambo wakati wa mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Julai 31, 2023 kuhusu mafanikio ya utendaji kazi wa  taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahariri wakiwa katika mkutano huo.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Jukwaa la Wahariri (TEF), Angela Akilimali akitoa neno la shukrani wakati wa mkutano UTT AMIS na Wahariri wa Vyombo vya Habari. Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

KAMPUNI ya UTT AMIS imejivunia mafanikio ya kiutendaji ambayo wamepata katika kipindi cha mwaka wa fedha ulioishia Juni 2023, mafanikio hayo yamekuja baada ya mfuko kufikisha Sh. trilioni 1.5 ikiwa ni sawa na asilimia 12.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa UTT Amis, Simon Migangala, alibanisha hayo leo, jijini Dar es Salaam katika Semina ya Wahariri wa vyombo vya Habari na alibainisha kuwa kutokana na utendaji wa Soko la Fedha lilivyo sasa hayo ni mafanikio na faida kubwa.

“Hali hiyo inatambulisha ukubwa wetu Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla wake tunaamini kwamba ndio tunaofanya vema kiutendaji na tutaendelea kufanya hivyo katika miaka ijayo hali itakayotufanya kuendelea kutoa gawio kwa Serikali kama ambavyo tumeweza kufanya tangu mwaka 2018 hadi sasa, amesema.  

Katika semina hiyo ambayo imeratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina yenye lengo la kuwafahamisha wananchi kuhusu kazi zinazofanywa na taasisi za Serikali, Migangala ameongeza kwamba kazi kubwa ya UTT Amis kusimamia mifuko ya uwekezaji wa pamoja ili kusaidia wawekezaji wadogo  kufikia fursa ya kuwekeza katika masoko ya fedha.

“Kwa kutumia mifuko hii mwekezaji mdogo akiwa na kiasi chochote cha fedha anaweza kuwekeza na UTT Amis kuweka katika masoko ya fedha na faida inayopatikana katika masoko hayo inarejeshwa kwa wawekezaji hivyo inasaidia mwekezaji mdogo kupata faida kubwa kama anayopata mwekezaji mkubwa,” amesema.

Ameongoza kuwa taasisi kama hiyo inapimwa kwa ukumbwa wa rasilimali ambazo inasimamia na katika kipindi cha mwaka mmoja imekuwa kutoka bilioni 996 hadi trillion 1.5 hivyo huo ni ukuaji ambao sawa na asilimia 54 na mwaka wa fedha ambao umepita walikuwa na ukuaji wa asilimia 50 baada ya kukua kutoka bilioni 600 hadi bilioni 996 hivyo kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita wamepiga hatua nzuri na ya kujivunia ya asilimia 50.

Amefanunua kuwa ukuaji huyo wa mafanikio yameenda sanjari na faida nzuri ambayo inapatikana kwa wawekezaji katika mifuko yote ya UTT AMIS ambapo kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2023 imekua na ukuaji wa zaidi ya asilimia 12 na kuonesha ubora mkubwa kwa wakezaji wote wakubwa na wadogo kwa kupata faida sawa.

Pia Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa UTT Amis, Daudi Mbaga, amesema kwamba katika kipindi cha miaka minne wamefanikiwa kupata mafanikio makubwa ambayo yanawafanya kutembea kifua mbele katika sekta hiyo.

Mbaga, ameongeza kuwa katika kufanikisha UTT AMIS, inaendelea kupiga hatua wamekuwa wakitoa elimu ya uwekezaji katika ngazi mbalimbali ikiwemo vyuoni na sasa wana mkakati wa kuhakikisha kuwa kwenye mitaala ya elimu linaongezwa somo hilo.

“Kwa sasa, UTT AMIS ndio habari ya mjini kutokana na wawekezaji kujitokeza kwa wingi kwetu na kipindi cha Covd kwetu kilikuwa ni kizuri kutokana na watu walikuwa wakiwekeza kwetu na kilitupa mafanikio,” amesema.

Ameongeza kuwa katika kufanikisha UTT AMIS inapiga hatua zaidi wanashirikiana na benki za CRDB, NMB, NBC na huku mikakati  mingine ikifanya kuhakikisha benki nyingi wanashirikiana nazo ili kutoa fursa kwa wananchi kujisajili kwa matawi na App za benki hizo.

No comments:

Post a Comment

Pages