Afisa ugania wa kituo cha utafiti cha Ilonga na mwezeshaji kutoka taasisi ya AMDT wakikagua zao la Alizeti la kuzalisha mbegu bora. Picha na Hamisi Adam.
Taasisi ya Uboreshaji wa Mifumo ya Masoko ya Kilimo (AMDT) itatoa mafunzo kwa maafisa ugani wa umma 1,340 kutoka wilaya 46 ili kuwawezesha kuinua zao la alizeti katika mikoa 18 nchini katika kipindi cha mwaka 2023.
Mafunzo hayo yanalengo la kuwafanya maafisa ugani hao kutoka katika wilaya hizo na taasisi za utafiti wa kilimo pia kuweza kuzalisha mbegu bora na kuwauzia wakulima wa zao la mikunde na alizeti ili waweze kuzalisha zaidi.
Taasisis hiyo pia imesema kuwa katika uwekezaji wake katika kilimo kwa kushirikiana na sekta binafsi imewezesha kuzalisha jumla ya kilo 26,000 ya mbegu ya alizeti aina ya Record iliyopandwa na kuoteshwa katika jumlya ya ekari 13,000 za zao la alizeti katika msimu wa kilimo wa 2022/2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa AMDT, Charles Ogutu alisema kuwa mbegu hizo tayari zimeshasambazwa katika taasisi za umma na kampuni binafsi zinazojihusisha na biashara ya mbegu nchini.
Ogutu amesema kuwa katika mwaka huu ADMT pamoja na mambo mengine pia itajikita katika kuwawezesha wakulima kulima kilimo cha mkataba na kusindika mazao yatokanayo na uzalishaji huo ili kuwawezesha kujipatia kipato zaidi.
AMDT ni taasisi inalenga kuisaida serikali kwenye vipaumbele vyake katika kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo nchini.
No comments:
Post a Comment