HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 09, 2023

TARI Ilonga kusaidia wakulima wadogo kurutubisha udongo

Wakulima wadogo wa wakiangalia zao la Alizeti lililostawi katika udongo uliopimwa na kurutubishwa katika kijiji cha Izava.Picha na Hamis Adam. 


 

 NA MIKE MANDE

 

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Kituo cha Ilonga kinafanya utafiti wa zao la mikunde inayosaidia kurutubisha udongo kuwawezesha wakulima wadogo kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Emmanuel Chilagane amesema kuwa utafiti huo utawezesha wakulima kutumia mbinu za kiasili na salama zaidi katika kurutubisha udongo.

 

Chilagane amesema kuwa kwa sasa wanafanya utafiti katika mazao ya mikunde ikiwemo marejea, karanga, maharagwe, kunde na njugu mawe ili kuweza kupata majawabu ya kutosha kuhusu mazao hayo na kazi yake katika kurutubisha ardhi.

 

“Tunafanya utafiti kutokana na mazingira mbalimbali na tabia za ardhi ya maeneo tofauti. Kiasili mazao hayo yamekua yakitumika katika kurutubisha ardhi. Ila kutokana na mabadiliko ya tabia nchi imetubidi kuangalia njia mbadala wa kurutubisha ardhi,” alisema.

 

Mtafiti na Mratibu wa Kitaifa wa zao la Alizeti Frank Reuben amesema kuwa utafiti utazingatia ushirikiano, mafunzo na ushamashishaji wa mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya hali yahewa ili kujenga ustahimili wa mazao mbalimbali.

 

Reuben alisema kuwa utafiti huo unawezeshwa na wadau mbali mbali toka sekta binafsi na taasisi za maendeleo chini ya ungalizi wa Taasisi ya Uboreshaji wa Mifumo ya Masoko ya Kilimo (AMDT).

No comments:

Post a Comment

Pages