HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 23, 2023

Benki ya CRDB yatoa msaada wa Madawati Kisarawe

 

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Fatma Nyangasa (wa nne kushoto), akikata utepe kuashiria makabidhiano ya Viti na Meza 50 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Shule ya Sekondari Msimbu iliyopo Kisarawe Mkoa wa Pwani.  

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msimbu wakiwa wamekaa katika viti na meza vilivyotolewa na Benki ya CRDB.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Fatma Nyangasa akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kupokea msaada wa Viti na Meza kutoka Benki ya CRDB pamoja na magodoro 50 pamoja na vitanda 100 kutoka ubalozi wa Uturuki kwa ajili ya mabweni ya wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Msimbu iliyopo Kisarawe.

Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Gongo la Mboto, Wemaeli Msechu, akitoa hoyuba yake wakati wa hafla ya kukabidhi Viti na Meza kwa Shule ya Sekondari Msimbu iliyopo Kisarawe.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Msimbu, Anicet Sauli, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya makabidhiano ya Viti na Meza 50 kutoka Benki ya CRDB.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe akiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa Benki ya CRDB pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.


Na John Marwa


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Fatma Nyangasa amepokea msaada wa vifaa mbalimbali vikiwemo viti na meza kutoka Benki ya CRDB kwa ajili ya shule ya Sekondori Msimbu.

Amewashukuru wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa michango mbalimbali na kipekee akiishukuru Benki hiyo kwa msaada huo.


"Kipekee niwashukuru Benki ya CRDB na wadau wote kwa ushirikiano wenu, kwa jitihada zenu ambazo mmekuwa mkifanya kuhakisha kwamba mnawasaidia watoto wetu wanakuwa kwenye mazingira mazuri, wanapata elimu yao katika mazingira mazuri na rafiki, tunawashukuru sana.

"Kisarawe kama Wilaya tumekuwa na changamoto mbalimbali kama maeneo mengine katika sekta yetu ya Elimu lakini serikali chini ya Raisi wetu, Mama yetu Dk. Samia Suluhu Hassan imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba Wilaya yetu inaboresha mioundombinu ya elimu.

"Hivi karibuni tumepokea kiwango cha fedha kama shilingi million 837 hivi, kiasi cha fedha hiki tumepanga kwa ajili ya kujenga madarasa pamoja na miundombinu mingine ya sekta ya elimu katika Wilaya yetu ya Kisarawe. Tumepokea fedha hizi na tuna kila sababu ya kumshukuru Mhe, Rais kwa fedha hizi."amesema na kuongeza kuwa.


"Bado tumekuwa tukipokea fedha mbalimbali kutoka kwa wadau na kutoka serikali kuu kwa ajili ya miradi mbalimbali katika sekta ya elimu, kwaiyo jitihada hizi na nyie kama wadau mnaziunga mkono kutusaidia katika maeneo mbalimbali zinatupa faraja kubwa Kwa kuwa na Imani kwamba tutafika mahali ambapo changamoto ndogondogo zitakuwa historia na watoto wetu watakuwa katika mazingira mazuri zaidi ya kupata Elimu yao na hatimaye kuzalisha watoto na vijana wenye tija kwenye jamii.

"Licha ya msaada tuliopokea leo lakini bado tuna changamoto nyingi kwenye Wilaya yetu tuna changamoto ya upungufu wa madawati, upungufu wa mabweni, vitanda kwenye mabweni na changamoto za miundombinu kwenye sekta ya elimu. Nichukue fursa hii kuwaomba sana, bado tunahitaji msaada wenu, bado tunahitaji mchango wenu, hapa tulipo tumemsikia mwalimu Mkuu akizungumzia changamoto mbalimbali ambazo bado zipo, kwaiyo tunaomba sana msituchoke kesho, keshokutwa." Amesema Nyangasa

Hata hivyo amewaasa wanafunzi walinufaika na msaada huo kuhakikisha wanautumia vema kwa kuzingatia usalama wa vifaa hivyo ili kuweza kutumika kwa muda mrefu.

"Kwenu nyie watoto wetu, leo tunakabidhiwa madawati, meza na viti pamoja na vitanda, magodoro na mashuka. Niwajibu wetu kuhakikisha kwamba tunatumia vitu hivi kwa uangalifu mkubwa Ili kesho meza unayopewa leo na Benki ya CRDB iendelee kuwepo atumie mwingine na kesho CRDB wakija waione wapate moyo wa kuleta nyingine." amesema Nyangasa.

Kwa upande wa Benki ya CRDB kupitia Meneja wa Tawi la Gongo la Mboto Wemaeli Msechu amesema benki hiyo ni mdau mkubwa wa elimu nchini jambo ambalo wanajivunia kutoa mchango wao katika sekta ya elimu.

"Benki ya CRDB kama mdau mkubwa wa Elimu, tunayo furaha pia kuwepo mahali hapa kwa ajili ya kutoa mchango wetu kwa ajili ya shule hii. Benki ya CRDB kama nilivyosema ni mdau mkubwa wa Elimu pia tunayo fursa ya kujumuika katika kuleta maendeleo ikiwemo pia kuchangia vifaa mbalimbali katika mashule yetu ya halmashauri zote Tanzania, na tumekwisha kufanya mengi.

"Tumeona tusiiache  Kisarawe katika kuchangia maendeleo ya elimu kwa kuchangia sisi pia ni wadau wakubwa katika maendeleo ya wilaya yetu ya Kisarawe.

”Kwa niaba ya Benki ya CRDB tuko hapa kama wawakilishi katika kutoa mchango wetu kama ulivyokwisha kutangazwa na mwalimu Mkuu, wa madawati, meza na viti hamsini kwa ajili ya kupunguza upungufu ambao uliokuwepo. Nachukua fursa hii kuupongeza uongozi wa Wilaya ya Kisarawe kwa kutuamini na kutuomba tuweze kufanya hili jukumu na leo tuko hapa kwa ajili ya kukabidhi. Niwaahidi tu kwamba bado tupo kwa ajili ya kusaidia maendeleo katika kukuza Elimu." Amesema Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Gongo la Mboto.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo shuleni hapo, Msimbu Sekondori ambapo Mkuu wa Wilaya Fatma Nyangasa amepokea msaada huo pamoja misaada mingine kutoka kwa wadau mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages