Mkuu wa
Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, Alex Mgeni (katikati) akimkabidhi
mfano wa
tiketi ya ndege Editha Kassim ambaye ni mmoja kati ya wafanyabiashara
10 wanaokwenda nchini China kwa ufadhili wa Benki ya NMB kwenda
kutembelea Viwanda, Biashara na Masoko ya Kimataifa. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam Agosti 1, 2023. Kushoto ni Meneja
Mwandamizi Idara ya Biashara NMB, Christopher Mgani. Hii ni mara ya Tatu
Benki hiyo inawapa fursa wafanyabiashara kujifunza zaidi kutoka wenzao
waliopo nchi za nje (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
Benki
ya NMB jana iliwaaga Wajasiriamali wadogo na wa kati 10 walioanza
safari ya kujifunza ya siku tisa jijini Guangzhou, China kwa udhamini wa
benki hiyo ilikijifunza mengi kutoka kwa taifa hilo ambalo limeendelea
kibiashara.
Wafanyabiashara
hao pamoja na mambo mengine wanatarajia kutembelea maonyesho ya
biashara mbalimbali kwaajili ya kujifunza masuala muhimu kwaajili ya
biashara zao na pia kutembelea viwanda na masoko.
Akizungumza leo
wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara
ya Biashara NMB, Alex Mgeni, alisema safari hiyo ni utekelezaji wa mkakati wa
benki hiyo unaolenga kuongeza thamani ya wateja wa benki hiyo huku
akisisitiza kuwa safari hiyo itawapa washiriki mwanga mpya katika
biashara zao.
“Kwa mara
nyingine tena, benki ya NMB inawatangazia ya kuwa leo tuna kwenda
kuwaaga wafanya biashara 10 ambao kwa udhamini wa benki ya NMB
watasafiri kuelekea nchini China kwaajili ya kutembelea maonyesho ya
biashara mbalimbali (Trade Fair) kwaajili ya kujifunza masuala muhimu
kwaajili ya biashara zao na pia kutembelea viwanda na masoko.
Tunatarajia
leo (jana) mchana wataanza safari yao kutoka uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea huko Guangzhou China, watapumzika
Dubai na kuondoka kwenda Guangzhou. Watawasili Jumatano Majira ya saa
nne usiku ya huko China. Hivyo wataanza rasmi Alhamisi ziara yao kwa
kutembelea Mangesh ya biashara,” alisema Mgeni.
Mgeni
alisema kuwa Benki ya NMB inaamini kuwa safari hiyo itakuwa na manufaa
makubwa sana siyo tu kwa wafanyabiashara hawa lakini pia kwa taifa kwa
ujumla.
“Sisi kama benki
ya NMB tunaamini kuwa ukuaji wa biashara zao utasaidia na kuchangia pato
la taifa, kuongeza ajira, hivyo ni manufaa kwetu sote,”alisema.
Mgeni
alisema kuwa benki yake imekuwa ikiwapeleka wafanyabiashara kipindi cha
nyuma hata kabla ya janga la korona huku akibainisha kuwa waka jana,
benki yake iliwapeleka wafanyabiashsra 10 nchini Uturuki.
“Mwaka
tunatarajia kupeleka jumla ya wafanya biashara 25. Tunaanza na hawa
10. Mwezi wa Oktoba tunapeleka wengine 15 kwenye Maonyesho maarufu ya
Canton Fair yanayofanyika huko huko China,” alisema.
Wakati
wa hafla hiyo, Editha Kassimu mfanyabiashara kutoka mjini Tanga ambaye
ni miongoni wa wafanyabishara waliopata fursa hiyo alishukuru benki ya
NMB kwa kuchangia ukuaji wa biashara yake tangu mwaka 2011.
“Nilanza
NMB mwaka 2012 baada ya kufungua akaunti kwa kiwango kidogo sana.
Niliweza kukopa na kununua mashine ya ushonaji kwa shilingi laki moja na
elfu 40. Najivunia kuwa na NMB kwa kuwa iliwezesha kuniwezesha na sasa
hivi hivi namiliki mashine za kisasa zaidi ya 20 na natoa ajira kwa
vijana wet,” alisema.
Aliongeza,
“Katika safari hii ya China, natarajia kujifunza zaidi hasa teknolojia
mpya na vitu vipya katika utendaji wa kazi yake,”
Alisema
baada ya kurudi nchini, anatarajia kutoa uzoefu atakaoupata kwa
wafanyabiashara wenzake ambao hawajapta fursa hiyo huku akiishukuru
benki hiyo kwa kuendelea kujitolea kuendeleza wafanyabiashara wadogo.
Mkuu
wa Idara ya Biashara wa Benki ya Alex Mgeni aliongeza kuwa benki hiyo
imeshirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini China kufanikisha safari
hiyo.
“Tumefurahi kuungana
tena na wateja wetu siku ya leo na hii ni kuunga mkono falsafa yetu ya
karibu yako. Leo ni mara ya tatu tangu tuanza zoezi kama hii. Wateja
wengi ambao wanasafiri wanafanya biashara ya vifaa vya ujenzi, vipuli na
biashara ya vipodozi,” alisema.
Aliongeza kuwa
wateja hao watapata fursa ya kujifunza mengi kwa kuwa nchi ya China ni
miongoni mwa nchi ambazo zimeendelea sana katika Nyanja hizo kwa kutumia
teknolojia.
“Tunatarajia
kuwa wafanyabiashara hawa watajifunza mbinu za kuzalisha kwa ubora na
mafanikio zaidi na kuongeza tija katika biashara zao,” alisema.
No comments:
Post a Comment