HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 01, 2023

KISA SIMBA DAY, WAUTAKA UWANJA WA UHURU

Na John Marwa

Uongozi wa Klabu ya Simba umeiandikia Serikali barua ya kuutaka Uwanja wa Uhuru kwa akili ya tamasha la wanasimba la Simba Day ''Unyama Mwingi' ambalo litafanyika Agosti 6 Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo Murtanza Mangungu katika uzinduzi wa hamasa kuelekea kilele cha Simba Day.

“Tumeandika barua kuiomba serikali itupatie na Uwanja wa Uhuru kwa kuwa tunaamini tutaujaza Uwanja wa Mkapa mapema tu.”- Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa klabu ameongeza kuwa.

"Tukio hili la Simba Day wengine wameiga ingawa hawataki kukiri hilo. Wameondoa neno Day wameweka Wiki."-amesema.


No comments:

Post a Comment

Pages