HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 05, 2023

Dola milioni 6 zajenge ghala la chakula

Na Richard Mrusha, Mbeya

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) imetumia dola za Marekani milioni 6.1 kwa ajili ya utekelezaji mradi mkubwa wa ghala la kuhifadhia chakula tani 21,000  katika Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa

 Mradi huo ni wa teknolojia ya kisasa na unatekelezwa katika Mikoa nane ya Tanzania ikiwemo Ruvuma, Songwe, Njombe, Rukwa, Katavi, Shinyanga Manyara na Dodoma.

Mhandisi wa Mradi huo Haruna Kalunga amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari hii leo Agost 4,2023 walipotembelea banda la TBA kwenye maonesho ya kimataifa ya kilimo Nane Nane 2023 yanafanyika kwenye Viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.



Mhandisi Kalunga amebainisha kuwa mradi wa ghala la kuhifadhia chakula Sumbawanga umeanza kutekelezwa mwezi Januari 2020 na umekamilika mwezi Machi 2023 na umeanza kutumika kwa kuhifadhi mazao ya chakula kwa wakulima.

"Mradi huo ni wa teknolojia ya kisasa, na unatunza chakula cha walicholima wakulima tani 21,000  na lengo kuu  la  mradi huo kutekelezwa kwa mikoa 20 lakini kwa sasa tumeanza na mikoa nane," amesema Haruna Kalunga.

Aidha Mhandisi Kalunga amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo na kufika katika banda la TBA ili kujua mambo mbalimbali ikiwemo gharama za ujenzi pamoja wa nyumba za makazi na taasisi za serikali kwa gharama nafuu.


No comments:

Post a Comment

Pages