Na Richard Mrusha, Mbeya
JESHI la kujenga Taifa Nchini(JKT) limewataka wananchi wa Mkoa wa Mbeya na Mikoa jirani kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye banda lake lililopo katika viwanja vya John Mwakangale ambako maonesho ya nane nane yanaendelea na kwamba wafike ili kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu shughuli za kilimo na kuongeza kuwa kwa upande wa shuguli zinazofanywa na jeshi hilo, ikiwa ni shirika la uzalishaji mali la Suma JKT pamoja na vikosi, shule na chuo.
Pia jeshi hilo limesema kuwa mbali na kutoa mafunzo katika nyanja za kilimo, mifugo na uvuvi lakini vilevile linatoa elimu kwa watanzania wote kuhusu sekta ya kilimo pamoja na mambo mengine.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa majeshi Nchini, pamoja na mkuu wa jeshi la kujenga Taifa,Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la kujenga Taifa Buligedia Hassan Rashid Mabena ameyasema hayo Jijini Mbeya Agost 1,2023 baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philp Mpango kuzindua maonesho hayo.
Kufuatia hali hiyo buligedia Mabena ametumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi hao kufika kwenye banda la JKT ambapo watajionea shughuli za kilimo ambazo zinafanywa, na jeshi la kujenga Taifa lenyewe linajihusisha na uzalishaji wa mazao ya chakula yakiwemo mazao ya mahindi, mpunga, Maharage pamoja na alizeti.
Alisema kuwa mazao mengine yanayozalishwa na jeshi hilo ni pamoja na mazao ya mbogamboga ambazo zinapatikana kwa wingi katika bustani zao lakini pia mazao ya biashara ya kimkakati kama zao la kahawa, chikichi, korosho pamoja na mkonge.
''Wananchi wafike hapa banda la JKt ili kujionea shughuli za kilimo zinazofanywa na jeshi hili lakini pia shughuli za ufugaji na uvuvi, jeshi la kujenga Taifa linajihusisha ufugaji wa mifugo ikiwa ng'ombe, mbuzi, kuku, lakini vilevile na ufugaji wa samaki lakini tunatoa elimu ya ufugaji wa samaki na nirahisi sana ambapo hata mfugaji ana eneo dogo sana na akaweza kuweza kufuga kisasa na akaweza kujipatia kitoweo lakini vilevile kuweza kujipatia mapato kuuza wale samaki ambao atawazalisha katika eneo lake dogo kwahiyo niwaase waje kwa wingi na kuweza kupata mafunzo hayo,''alisema Buligedia Mabena.
Aliongeza mafunzo hayo yanatolewa kwa vijana kupitia wataalamu wa kilimo wa jeshi hilo na kubainisha kuwa mafunzo yanatolewa kwa kundi la vijana wa lazima kwa maana ya mujibu wa sheria na lile kundi la vijana wa kujitolea.
No comments:
Post a Comment