HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 02, 2023

MKINGA FOUNDATION WAPONGEZWA KUWEKEZA KWENYE JAMII ZENYE UHITAJI


Katibu wa Shirika la Mkinga Joseph Kibena akikabidhi Vipaza sauti kwa viongozi wa Msikiti wa Likarangiro.

 

NA STEPHANO MANGO, MADABA

 

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mkoani Ruvuma Wakili Sajidu Mohamed amelipongeza Shirika la Mkinga Foundation kwanamna linavyofanya kazi zake kwa lengo la kuisaidia Serikali kwa kufadhiri mambo mbalimbali kwenye jamii zinazoizunguka Madaba

Wakili Mohamed akitoa shukrani hizo hivi karibuni kwa wadau wa Maendeleo ambao walifanikisha maadhimisho yay a siku ya Mtoto wa Afrika ambayo kiwilaya yalifanyika katika Kijiji cha Matetereka alisema kuwa shirika hili ni dogo na jipya lenye dhamira ya kuigusa jamii yote ya watu wa Madaba, Mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla.

Alisema kuwa kwa muda mfupi shirika hilo limeweza kuifikia jamii yenye uhitaji na kwamba mchango wake unatambuliwa na Halmashauri hiyo,  hivyo alilitaka Shirika hilo kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta ustawi kwa jamii pana zaidi

Alieleza kuwa uwepo wa Asasi za Kiraia ni muhimu kwa ukuaji wa demokrasia na utawala bora katika nchi yetu, hivyo nawapa hongera sana kwa kazi zenu ambazo mnazifanya katika jamii, Serikali ipo pamoja nanyi katika kutimiza adhima yenu

Kwa upande wake Katibu wa Shirika la Mkinga Joseph Kibena alisema kuwa hadi sasa limefanikiwa kutoa spika hizo zenye thamani ya Tsh. 875,000/= baada ya kupokea maombi kutoka kwa viongozi wa msikiti Kiislamu wa kijiji cha Likarangiro kata ya Mtyangimbole

Kibena alisema kuwa hivi karibuni tumeweza kutoa mabenchi ya kukalia abiria kwenye kituo cha mabasi cha ambayo yamegharimu Tshs 420,000/= pia , tumefanikiwa kugawa miche ya parachichi, kusapoti michezo kwa kutoa jezi kwa vilabu 8 vya mpira wa miguu Madaba

Alisema kuwa Shirika hilo limeweza kushiriki shughuli zinazoandaliwa na Serikali kama vile siku ya Mtoto wa Afrika, kuchangia katika harambee mbalimbali za ujenzi wa miradi ya Serikali na jamii kama vile makanisa na misikiti na kusaidia walemavu, kusaidia vikundi vya ujasiliamali na mambo mengine mbalimbali katika jamii

Kibena alieleza kuwa Shirika limeahidi kuendelea kushirikiana na kuiunga mkono Serikali na viongozi katika kutatua na kupunguza changamoto za wanajamii ili kuleta maendeleo.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Waumini wa dini ya Kiislamu wa kijiji cha Likarangiro kata ya Mtyangimbole wamelishukuru sana  Shirika la Mkinga Foundation kwa kuwapa Spika za matangazo kwenye msikitini wao.

Shukrani hizo zimetolewa na Imamu wa msikiti wa Likarangiro Rashid Mwenda na Mzee wa msikiti, mzee Zuberi kwa niaba ya waumini wote na kwamba wameliweka mikononi Mwa Mwenyezi Mungu Shirika hilo ili liweze kutimiza malengo yake

No comments:

Post a Comment

Pages