HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 01, 2023

MASHINDANO YA MBUNGE CUP YAFIKIA PATAMU

 

Na John Marwa


Mashindano ya Mbunge Cup Jimbo la Ukonga maarufu kama Nane Nane Cup yamefikia patamu baada ya kupata timu za robo fainali ngazi ya vijana.


Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya michezo iliyopigwa leo katika viwanja mbalimbali jimboni humo jioni ya leo.



Timu ya Naweza Youth imeifulusha mabao (3 - 0) Jagwa FC, Chanika City nao wametinga Robo Fainali kwa kuwaondosha kwa mikwaju ya penati (4-3) dhidi ya Wala Mboga FC,  Majohe United dhidi ya Kipunguni (hawakufika Uwanjani sababu ya msiba).


Wakati Chakenge wamitungua mabao (4-2) Msongola, Buyuni United wamewatupa nje Pugu United kwa mikwaju (5-4), Goms United wao wamefungisha virago vyao kwa penati (3-4) dhidi ya Pugu Stesheni.


Washindi wa michezo hiyo hapo juu wametinga Robo Fainali ya Jerry Silaa, Mbunge Cup ama Nane Nane Cup 2023 Jimbo la Ukonga ambapo hatua hiyo itapigwa Agosti 8 na kuaptikana washindi wa michezo hiyo na michezo mingine inayofanyika katika Bonanza hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages