HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 01, 2023

MSAJIRI AWAKUMBUSHA WANASIASA KUZINGATIA SHERIA


NA MWANDISHI WETU

 

VYAMA vya Siasa nchini, vimekumbushwa kuzingatia kanuni na sheria ambazo zimetungwa ili kuleta amani na utulivu na wakisisitizwa kutumia lugha ya stara.

 

Pia wanasiasa wamekumbushwa kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia masuala ya siasa nchini ili kutoleta mpasukakatika jamii.

Hayo yamezungumzwa leo jijini Dar es Salaam na Jaji Francis Mutungi wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili mwenendo wa siasa nchini ulioandaliwa na Baraza la Vyama  vya Siasa.

 

“Wakati mwingine wanasiasa mnafanya mikutano ya ndani ambapo maofisa wetu huwa hawapo jambo ambalo wakati mwingine linapelekea kutoa lugha ambazo si sahihi kitu ambacho ni hatari kwa maslahi ya nchi.

 

“Ofisi ya Msajili si Polisi hivyo kama kuna changamoto yoyote imejitokeza katika shughuli zenu mnakaribishwa wakati wowote kwani tunajenga nyumba moja hakuna haja ya kunyang’ana fito,” amesema.

 

Pia naye Mwanasiasa mkongwe, John Cheyo amesema kuwa kikao hicho nia yake ni kujenga uhusuano mzuri kwa watanzania ambao siku zote wanahitaji amani na utulivu.

 

“Nimekua kwenye siasa kwa kipndi kirefu na nimezunguka katika mataifa mbalimbali na sikuona mwanasisasa aizungumzie vibaya nchi yake lakini kwa sasa nashuhudia baadhi ya wanasiasa hapa nchini wakiizungumzia vibaya nchi yetu nje ya mipaka ya Tanzania, tunakwenda wapi?, amehoji.

 

Naye Padri, Florence Rutaiwa ambaye ni Mkurugenzi wa Kurugenzi Kichungaji kutoka Baraza wa Wachungaji, amesema wao wakiwa ni sehemu ya viongozi wa dini kazi yao kubwa kushauri wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu zinazompendeza Mungu.

 

Hivyo wakati wowote wanapoona wanasiasa wanakengeuka watawaona kupitia kwenye nyumba zao za ibada ili wafanye siasa safi kwa ajili aya kulinda amani ya nchi na si kupanda majukaani.

 

Viongozi wa dini kazi yetu ni kuhakikisha tunakemea dhambi kwa yeyote anayekengeuka katika majukumu yake ya kisiasa bila kumuonea mtu, amesema.

 

  Kwa upande wake, Amiri Mkuu wa Baraza Kuu na Jumuia za Taasisi za Kiislamu Tanzania Mussa Kundecha, amesema kwamba wakati mwingine ni vigumu kutofautisha shughuli za kisiasa na masuala ya dini kutokana na kwamba yote yanahusiana na usimamizi na mambo ya kijamii.

 

Hivyo mwanasiasa naye anajihusisha na mambo ya kijamii ingawa Siasa ina vigawo vingi, hivyo kiongozi wa dini si vema kujihusisha na siasa kutokana na kwamba inawezekana waumini wake wapo katika makundi tofauti ya vyama hivyo akijiingiza anaweza kuwaganya na kuleta machafuko.

 

Pia alibanisha kuwa dhambi ya kisiasa ni kubwa sana kwa maana inaweza kuathiri watu wengi kutokana na kwamba mtu anayetaka uongozi anaweza kuua watu wengi ili apate uongozi, hivyo inastahiri kukemewa kwa nguvu kubwa.

No comments:

Post a Comment

Pages