Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda akizungumza kwenye ufunguzi wamafunzo ya Uongozi kwa viongozi leo Julai 31 kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo maeneo ya ya Kwamfipa wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Na Khadija Kalili
WAZIRI Mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda leo amefungua mafunzo kwa Viongozi kutoka katika Taasisi mbalimbali za seeikali mafunzo hayo ya Uongozi na Maadili yanayofanyika kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Akifungua mafunzo hayo leo Julai 31 wa Chama na Serikali kujiendeleza na elimu ya Uongozi ili waweze kuwasimamia vyema wanaowaongoza katika sehemu zao za kazi huku amesema kuwa kwamba elimu haina mwisho.
Amesema kuwa upo umuhimu wa akitoa wito wa kuwaendeleza wataalamu mbalimbali kwa lengo la kuwajengea uwezo ,uzalendo wa nchi yao jambo ambalo litachochea wqtu kufanya kazi kwa bidii, juhudi,maarifa makubwa na kutojali kuona wanapoteza nguvu zao kwa kiasi gani.
"Uzalendo ni dhana yenye wigo mpana zaidi hivyo jambo hili ni la muhimu mtu kukaa darasani na kupikwa ili pindi anapomaliza mafunzo haya atoka akiwa ameiva na kuelewa dhana halisi ya kua mzalendo ndani ya nchi yako, zamani viongozi walipikwa pindi walipoteuliwa tofauti na ilivyo sasa hivyo ili kuongeza ufanisi katika uongozi nashauri viongozi wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na watu wa kada mbalimbali wawekewe utaratibu wa kupata mafunzo kama haya mara kwa mara"amesema Mheshimiwa Pinda.
Akifungua mafunzo hayo ya wiki moja Mheshimiwa Pinda amesema kuwa amefurahishwa kuona uwiano wa washiriki wa mafunzo hayo ambapo jinsia zote zimeshirikiswa ipasavyo.
Amesema kuwa wakati umefika wa kuwajengea uzalendo wananchi wa kada zote wakiwamo wanafunzi huku akitolea mfano wa nchi ya Izrael namna ambavyo wamewajengea wananchi wao kuipenda na kuithamini nchi yao huku akisema kuwa kila Mtanzania anapaswa kuwa mzalendo licha ya kuwa na itikadi tofauti za kidini, kabila na rangi lakini wote wawe kitu kimoja.
Ametoa sifa kwa uongozi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere kuwa licha ya kuwa hakina muda mrefu lakini matunda yake yameanza kuonekana na maua yake yamechanua kutokana na mafunzo waliyopatiwa watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa , viongozi wa ndani na nje ya nchi.
"Viongozi wangu katika serikali naomba tuwajibike kikamilifu, kwanza wajibika halafu dai haki yako kila Kiongozi anapaswa kuwa mbunifu na mzalendo katika Taasisi yake na kuwajibika ipasavyo.
"Mashirika makubwa na Taasisi nyingi za serikali zinayumba sababu Viongozi wengi siyo waadilifu,kitu kinachoitwa uadilifu ni kigumu lakini endapo utakaa na kina babu ambao ni wakongwe kuna mambo mazuri unaweza kuyapata binafsi naweza sema nimepata bahati ya kufanya kazi na viongozi wakongwe wengi ambao ndiyo walionijenga natumia mfano huu ikiwa ni lengo la kutaka kuwakumbusha umuhimu wa kuthamini wazee katika utendaji wetu" amesema Pinda.
"Nasisitiza uadilifu na kuacha maovu ambayo yanaathiri jamii kwa ujumla ndiyo maana CAG akitoa ripoti yake inakua imejaa madudu mengi yote haya ni kutokana na upungufu wa maadili ya uongozi kwa baadhi ya viongozi nchini ". amesema Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Pinda.
Ametoa rai kwa uongozi wa Shule ya Mwalimu Nyerere kuwepo na utaratibu wa kutoa mafunzo mafupi yanayohusu uongozi, uzalendo na uendeshaji nchi kwa ujumla .
"Wateule wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jipangeni ili mje kupata mafunzo hapa itumieni fursa ya Shule hii ya siasa kuwapika makada wa chama ili waweze kukinadi chama kwa weledi wa hali ya juu"amesema.
Mkuu wa Shule hiyo ya Mwalimu Nyerere Prof.Marceline Chijoliga amesema kuwa wanajivunia kwa kutoa mafunzo bora kwani hadi sasa tayari zaidi ya wahitimu 2,000 wamepata mafunzo katika Shule hiyo.
"Mapema mwezi huu jumla ya viongozi wanawake 71 wamehitimu mafunzo yaliyowashirikisha washiriki kutoka katika Taasisi mbalimbali nchini na wamehitimu vyema hivyo tunatarajia watakua viongozi bora huko waliko, mafunzo waliyopata yamewajengea uwezo viongozi hao wanawake na ambao wanauzoefu siyo chini ya miaka mitano ambayo yamefanyika kwa mara yakwanza hapa nchini ambapo wahitimu wamefundishwa mbinu bora za Uongozi wa Utawala Bora katika Taasisi wanazoziongoza.
Aidha ufunguzi huo umehudhuriwa na viongozi wa chama na serikali akiwamo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon , Mwanasiasa Mkongwe nchini ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali Mzee Paul Kimiti.
Mstaafu Paul Kimiti amewahimiza viongozi hao kuwa wazalendo ndani ya nchi yao.
Amesema kuwa hakuna aliye juu zaidi ya mwingine hivyo amesisitiza kuwa kila mmoja anamtegemea mwenzake na kusema kuwa katika maisha epuka kufanya maamuzi katika jambo lolote bila kushirikisha wenzako wengine wanao kuzunguka kwani hiyo ndiyo sifa ya Kiongozi bora.
"Kiongozi bora huheshimu anaowaongoza na kuwashirikisha bila ya kujali umri ,itikadi zao za dini na mambo mengineyo yanayowatofautisha.
No comments:
Post a Comment