HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 01, 2023

Waziri Makamba azindua Mpango Mkakati wa TANESCO wa Miaka 10

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Waziri wa Nishati January Makamba amezindua Taarifa ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 na Mpango Mkakati wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wa Miaka 10.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika leo jijini humo, Waziri Makamba amelipongeza TANESCO kwa hatua nzuri kuelekea mabadiliko makubwa ya Shirika ambayo hayajapata kutokea.


“Hii haijapata kutokea, sisi tunachoomba kwa wananchi, wadau na wateja Wetu ni kuwa na subira, kwani mabadiliko yanahitaji muda mrefu,” amesema Waziri Makamba na kuongeza,

“Mabadiliko yanayofanyika TANESCO yanaweza yasieleweke haraka,”.


Waziri Makamba amebainisha kuwa kama Serikali wataendelea kuliunga mkono shirikisho hilo ili kufikia malengo na mipango ya TANESCO.


Hivyo amesema kwamba Serikali inafanya juhudi ya kuitafimutia Mtaji wa kutosha ili kufikia malengo yake.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Maharage Chande, akieleza kuhusu mafanikio kwa Mwaka wa Fedha 2021/2023, amesema kwamba Shirika limeweza kupata faida ya Sh Bilioni 109.


Kadhalika wameweza kuanzisha namba moja ya huduma kwa wateja, kuunganisha wateja 504,366, kupungua kwa upotevu wa Umeme kutoka asilimia 14.5 hadi asilimia 15 lengo lililowekwa.


Kwamba wanaendelea kuitekeleza Miradi ya kimkakati ukiwemo Mradi wa Mwalimu Julius Nyerere ambao umefikia asilimia 90.


Akizungumzia kuhusu Mpango mkakati wa miaka 10 ijayo, Chande amesema wamejipanga kuwekeza kufanyakazi kidigitali, kuongeza juhudi za kutatua changamoto za wananchi na kuhakikisha kuna mtiririko mzuri wa kifedha.

Nae, Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Omary Issa ameeleza kuwa Shirika linamkakati mkubwa wa kuandaa Vijana watakao kuja kuliendesha kwa miaka ijayo.


Hivyo amesema kwa sasa kuna kikundi cha watu kiko nje ya Nchi kikipata mafunzo na kwamba hawataishia kwa kikundi hicho tu bali wataendelea na kwa wengine.


 

No comments:

Post a Comment

Pages