HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 09, 2023

MKUTANO WA CHAKULA KUFANYIKA KWA MARA YA KWANZA TANZANIA KUWA MWENYEJI

Na Magrethy Katengu


Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa kimataifa wa chakula unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es salaam kuanzia Agisti 10-12 Mwaka huu katika ukumbi wa Daimond Jublee unaotarajiwa kuhudhuriwa na Makampuni zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya nchi ya Wafanyabiashara, Wakulima na Wazalishaji .


Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa  Pulses Ntwork (TPN) Zirack Andrew   Jijini Dar es salaam amesema katika siku hizo kutakuwa na mabanda ya maonyesho ya aina tofauti tofauti ya mazao ya chakula kutoka katika  kampuni mbalimbali hivyo kutakuwa  kongamono na midahalo mbalimbali na mainyesho na kunatarajia zaidi ya watu 3000 kutembelea mabanda kujifunza fursa zilizopo katika uzalishaji mazao ya chakula kupitia teknolijia ya juu kutoka nchi za nje hivyo ni vyema wakulima kuhudhuria ili  kubadilishana uzoefu .


" Huu ni Mkutano unaofanyika kwa mara  kwanza  Afrika na mara ya kwanza Tanzania vyama tofauti tofauti vya vyakula Afrika tumeshirikiana  kuwaleta wenzetu toka India. waliokuwa na uzoefu kufanya maonyesho kama haya miaka mingi sana India, Mashariki ya kati na sehemu nyingine tofaui tofauti Duniani ili kupata uzoefu na kuunganishwa na  fursa ya kupata  masoko ya kimataifa uuzaaji mazao ya chakula" amesema 


Andrewa amesema Dhima ya Mkutano huu kimsingi ni kufungua masoko ya mazao Afrika nzima na duniani kote kiujumla kwani miaka mingi iliyopita wakulima walikuwa wanalima mazao kwa ajili ya kujikimu wao na familia zao siyo kuuza lakini miaka michache ya sasa  Wamehamia kutoka katika kilimo cha kujikimu na kulima kilimo cha kibiashara na imekuwa na matokeo chanya kuongezeka sana kwa mazao ya chakula.



Naye  Miongoni mwa Jopo la Waandaji wa Mkutano huo kutoka nchini India Mkurugenzi wa Taso Event Suveer Rajapuexlint amebainisha kuwa nchi nyingi za India, Asia, Mashariki ya kati na China zina idadi kubwa sana ya watu lakini pia kipato chao cha mtu mmoja mmoja ni kikubwa sana akitolea mfano China ni nchi ya pili kwa uchumi mkubwa  pia India inaenda kwa kasi uchuminwake hivi juzi juzi miezi miwili iliyopita India imeipita Uingereza kuwa ya ni nchi ya 5 kwa uchumi mkubwa Duniani ina maana kuwa kipatao cha mtu mmoja mmoja  kimezidi kuongezeka  hivyo nao wananunu chakula kutoka Tanzania. 



"Mazao yakiwa mengi na masoko hayapo inakuwa changamoto hivyo tumeangalia kuwa Kuna sehemu Duniani wanakuwa na uhaba wa chakula lakini taarifa ya uzalishaji wapi watanunua chakula hawana  hivyo kupitia kongamano na mkutano huu sambamba na maonyesho  itasaidia wakulima kuunganishwa na wanunuzi wa mazao kutoka nchi ikiwemo  Asia, India, na china  Mashariki ya kati "Suveer


Aidha watu wote wanakaribishwa kuweza kuhudhiria Mkutano huo kwani kutakuwa na muda wa midahalo tofauti tofauti kutoka katika mazao ya aina mbalimbali pia


wafanyabiashara watakutana kuzungumza kwa pamoja na kuingia makubaliano ya kibishara ya siku chache za usoni hivyo vikundi vya wakulima wafanyabiashara na watajionea fursa ya teknolojia kutoka nje na kubadilishana uzoefu

No comments:

Post a Comment

Pages