HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 09, 2023

IZAKU Amcos yajikita zaidi kuzalisha mbegu bora ya Alizeti

 

 Akina mama kutoka katika kijiji cha Kapumpa wakichambua mbegu bora ya Alizeti iliyplimwa kwa mkataba.Picha na Hamis Adam.

 

NA MIKE MANDE

 

Chama cha ushirika cha msingi cha IZAKU (Izaku-Amcos) kitajikita zaidi katika uzalishaji mbegu bora ya Alizeti aina ya Record katika msimu wa kilimo wa 2023/2024 ili kuweza kuwasaidia wakulima wa ushirika huo kupata mbegu kwa bei nafuu na kulima zaidi.

 

Mwenyekiti wa Ushirika wa IZAKU, Omari Issa amesema kuwa ushirika huo pia utawezesha wakulima kulima zao la Alizeti kwa wingi ili kiweze kukamua mafuta katika kiwanda kinachomilikiwa na ushirika huo na katika msimu wa 2023/2024 inategemea kulima ekari 3000.

 

Issa pia alisema kuwa IZAKU imeshaingia mkataba na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) ili kununua Alizeti yote iliyozalishwa na ushirika huo katika msimu wa kilimo wa 2022/2023.

 

Ushirika wa IZAKU unaundwa na vijiji vitatu vya Umoja, Izava na Kimeji na kina wanachama wasiopungua 10,000.

No comments:

Post a Comment

Pages