Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Deogratius Ndejembi akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura (Elimu), Bi.Monica Mnanka aliyekua akimpa Elimu ya Wapiga Kura wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika viwanja vya Nzuguni yanapofanyika maonesho ya Wakulima Nane Nane Kanda ya Kati, Dodoma leo Agosti 6,2023.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura (Elimu), Bi.Monica Mnanka akimpa maelezo namna uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linavyofanyika katika viwanja vya Nzuguni yanapofanyika maonesho ya Wakulima Nane Nane Kanda ya Kati, Dodoma leo Agosti 6,2023.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Tume waliokuwa katika banda hilo la Tume.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za mkoani Dodoma ni miongoni mwa wadau wanaotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwaajili ya kujifunza masuala mbalimbali ya uchaguzi.
Afisa wa Tume kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Sheria, Jamila Mziray akimsikiliza mwananchi aliyetemberlea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura (Elimu), Bi.Monica Mnanka akitoa Elimu ya Mpiga Kura. Afisa wa Tume, Bi. Johari Mutani (kushoto) ambaye ni Mtaalam wa Lugha ya Alama akimsikiliza mdau wa uchaguzi mwenye ulimavu wa uziwi aliyetembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi, viwanja vya Nzuguni Dodoma yanapofanyika maonesho ya Kilimo Nane Nane.
No comments:
Post a Comment