*Asisitiza ushirikiano baina ya Serikali na Sekta binafsi katika utoaji huduma za kitalii
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)(wa tatu kushoto) akizungumza na wahudumu wa hoteli ya Home Ground ambapo amewataka kuwa wakarimu wanapohudumia wageni ili kuwavutia waweze kurudi kwa mara nyingine. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Hoteli ya Home Ground, Bw. Kevin Mbogo na kushoto kwake ni Mbunge wa
Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Taska Mbogo.Wengine ni baadhi ya
viongozi wa Chama na Serikali wakishuhudia.
Naibu Waziri wa Maliasili
na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)(katikati), Mkurugenzi
Mtendaji wa Hoteli ya Home Ground, Bw. Kevin Mbogo(wa pili
kushoto) pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali
wakikaguamojawapo ya chumba cha hoteli ya Home Ground kabla ya uzinduzi
wa hoteli hiyo uliofanyika katika Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi jana.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb),akizindua Hoteli ya Home Ground. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi Mhe. Willian Mbogo pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wakishuhudia uzinduzi huo uliofanyika katika Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi jana.Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Home Ground, Bw. Kevin Mbogo wa pili kutoka kuli) pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali.
Na Mwandishi Wetu
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amezindua hoteli ya
Home Ground katika Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi itakayosaidia kukuza
Mtandao wa Utalii katika eneo la huduma na malazi kwa watalii wanaokuja
nchini.
Akizungumza jana
Agosti 6,2023 katika uzinduzi huo, Mhe. Masanja amesema kuwa uwekezaji
wa hoteli hiyo unaenda kusaidia Hifadhi ya Taifa Katavi ambayo ni moja
kati ya hifadhi ya tano kwa ukubwa nchini ikiwa yenye kilomita za
mraba 4,471.
Ameongeza
kuwa uzinduzi wa hoteli hiyo ni mwendelezo wa ushirikiano baina ya
Serikali na Sekta Binafsi katika utoaji wa huduma za malazi nchini.
“Tukio
hili linaonesha dhahiri umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na
sekta binafsi katika kutoa huduma za kitalii na pia linaunga mkono
juhudi thabiti za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kama alivyoeleza katika
uzinduzi wa filamu ya "The Royal Tour " *“tunapenda kuwakaribisha
wawekezaji wengine kwani Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutangaza
utalii duniani na kufungua milango kwa nchi nyingi kutembelea Tanzania* ”
Mhe. Masanja amesema.
Aidha,
ametumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa uwekezaji huo mkubwa
uliofanyika, huku akisema idadi na viwango vya huduma za malazi
imeongezeka.
"Sisi kama
Serikali tutazidi kuweka mazingira wezeshi ili kudumisha ushirikiano
mkubwa katika kukuza na kuongeza idadi wa watalii wanaofika katika
hifadhi hii ya Katavi, wekezeni kwenye huduma za malazi " amesisitiza
Mhe.Masanja.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi wa Hoteli ya Home Ground, Mhe. William Mbogo
amesema ujenzi wa Hoteli hiyo uliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.5
ulianza mwaka 2019 na unatarajiwa kutumia takribani bilioni 4 mpaka
kukamilika kwake.
Amesema
uwekezaji huo utasaidia kuchangia katika mapato ya Serikali kwa kodi
mbalimbali inayolipa lakini pia umetoa ajira kwa vijana takribani 40 wa
Kitanzania.
Mbogo
ametumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuboresha miundombinu ya Hifadhi ya
Taifa ya Katavi pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji
wanaotaka kuwekeza ndani ya hifadhi hiyo.
No comments:
Post a Comment