Mwanamuziki
wa dansi nchini, Jonhson Nguza ‘Papii Kocha’ amesajiliwa na
kutambulishwa kama Muimbaji wa Bendi ya Town Classic kwa lengo la
kuongeza nguvu katika bendi hiyo.
Mbali
na Papii Kocha bendi hiyo imesajili wanamuziki wengine ambao ni Amri
Francis na Fayed Basizi pamoja na Mpigaji wa solo Elombe Kichinja.
Mkurugenzi wa bendi hiyo, Pactrick Kessy amesema usajili huo utaleta tija katika kukuza tasnia ya muziki na bendi yao kiujumla.
“Tumemsajili
Papii Kocha na wenzake kwa lengo la kuja kupambana na kuongeza nguvu
katika bendi yetu, pia kurudisha hadhi ya muziki wa dansi."
Patrick amewata mashabiki wa bendi hiyo wategemee kuona mambo mazuri kutoka kwao, pia nyimbo zenye ushindani zikitungwa.
Mkurugenzi
huyo ameongeza kuwa Septemba 9 mwaka huu watamtambulisha Papii Kocha
katika Kijiji cha Makumbusho kilichopo Dar es Salaam
Mwanamuziki, Papii Kocha amesema mashabiki wa muziki wa dansi na wategemee nyimbo zenye maudhui mazuri kutoka kwake.
“Nitahakikisha
hadi ikifika miezi sita nitakuwa nimetunga nyimbo ambazo zitakuwa
katika mfumo wa ablamu ambazo zitaleta ushindani katika tasnia ya muziki
nchini."
Papii
Kocha ambaye alitamba na ngoma ya ‘Seya’ ilifanya vema hapo awali
alikuwa katika bendi ya Tukuyu Sound akishirikiana na Kalala Junior.
No comments:
Post a Comment