HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 05, 2023

RC MTAKA: DHANA YA KILIMO BIASHARA INABEBWA NA COSTECH

MKUU wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, ameipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kutokana na kubeba dhana ya Kilimo Biashara ikiwemo kuwa taasisi inayosaidia watafiti na wabunifu.


Mtaka amesema hayo alipotembelea Banda la COSTECH katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nane Nane 2023) yanayoendelea kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.


Mbali na hayo, Mtaka ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuuwisha COSTECH na kuendeleza Tafiti na Bunifu zinazofanywa na Vijana katika maeneo mbalimbali hapa nchini.


Vilevile amesema kwenye mageuzi ambayo Serikali inafanya sasa hususani maamuzi ya  Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kutamani nchi iwe inalisha bara la Afrika ni kuwaendeleza watafiti na wabunifu wakazalisha bidhaa zenye tija zitakazoinua Taifa letu kiuchumi.


Mtaka amezishauri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Kilimo, kushirikiana ili kuendeleza Teknolojia zitakazowezesha kufanya vizuri zaidi.

Ameipongeza COSTECH kwa kuendelea na kukuza Tafiti na Bunifu ikiwemo kuwashauri Wananchi, washiriki na viongozi kutembelea Banda la tume hiyo ambako watajifunza mengi.


Mtaka amewaalika COSTECH kushiriki Maonesho ya Viwanda Vdogo Vidogo (Sido) yatakayofanyika mkoani Njombe, ambapo COSTECH watakuwa wadau wakubwa na kusaidia kuwaalika vijana kushiriki Maonesho hayo.

No comments:

Post a Comment

Pages