Na John Marwa
KOCHA Mkuu wa klabu ya Simba, Robert Oliveira 'Robertinho' ametamba kuwa wachezaji wake wako tayari lakini kutembeza dozi kwa wapinzani wao kwenye mashindano mbalambali yaliyoko mbele yao.
Amesema kundi la wachezaji wa kwanza wako tayari kwa mapambano ya mashindano yaliyoko mbele yao lakini bado anahitaji kupata muda zaidi wa kuupata muunganiko wa timu nzima ili kuendeleza rekodi ya matokeo mazuri katika mashindano yote.
Katika mchezo huo Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliofungwa na Willy Essomba Onana na Fabrice Ngoma.
"Kambi yetu imetusaidia kwa sababu tumeweza kuimarisha eneo la kiungo kwa sababu nilikuwa na makundi mawili ya kuwasoma wachezaji, ukiangalia kama Ngoma amecheza vizuri japo haikuwa rahisi kutengeneza uelewano kwa timu mpya, Lakini baada ya mchezo nimeongea na Kibu (Denis), Saido (Ntibanzokiza) na Chama (Clatous) kuwa ushirikiano ni bora waliofanya na kupelekea kupata matokeo mazuri.
"Sasa tunajiandaa na Supa Ligi kwa sababu timu ya kwanza ipo tayari ingawa haiwezi kunifanya nibadili timu ya kwanza haraka japokuwa bado nahitaji muda zaidi wa kuweza kuijenga timu ya pili na kuweza kupata muunganiko wa timu nzima ambao utasaidia kuonyesha soka ambalo nalitaka lichezwe hapa kwa lengo la kupata matokeo mazuri katika michezo ambayo tutacheza," amesema Robertinho.
Kwa upande wa kocha Power Dynamo, Mwenya Chipepo alisema nafasi waliyoipata kucheza na Simba kwao kilikuwa kipimo sahihi kuelekea katika michuano iliyopo mbele yao huku akiwapongeza Simba kwa kuweza kuonyesha kiwango kizuri kwenye mchezo huo.
No comments:
Post a Comment