HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 03, 2023

Sita wakamatwa kwa uharibifu wa mazingira Same

 Na Mwandishi Wetu, Same

WATU sita wa kata ya Mhenzi wilayani Same mkoani  Kilimanjaro wamekamatwa kwa kuhifadhi wachimbaji madini zaidi ya 70 ambao walikuwa wanaharibu vyanzo vya maji.

Zoezi la ukamataji watu hao limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Same , Kaslida Mgeni katika ziara yake ya kushtukiza ambayo aliambatana na Kamati ya Usalama ya wilaya hiyo.

Katika ziara hiyo ya kushtukiza  kwenye vyanzo vya maji wachimbaji hao wa madini wamesababisha wananchi kukosa maji safi na salama.

Kaslida amesema kitendo cha wachimbaji hao kufanya shughuli za uchimbaji kwenye vyanzo vya maji no kinyume cha sheria na uharibifu wa miundombinu ya maji na kuhatarisha maisha ya wananchi kutokana na  kusafishia madini kwa kutumia mercury ambayo ni hatari kwa binadamu.

Mkuu huyo aliwataja watu waliokamatwa Sallum Shaibu, John Vicent, Husein Mussa na Peter Joseph wote wakiwa wakazi kata wa Mhenzi.

Alisema chanzo hicho cha maji kilichoharibiwa kinategemewa na wananchi zaidi 22,000 wa kata  nne za Vudee, Mwembe, Mhezi  na Mbangalala.

DC Kasilda watu hao sita wamekuwa wakiwafadhili wachimbaji hao kwa vitendea kazi na mahitaji mengine muhimu.

Amesema serikali haitavumilia mtu yoyote ambaye anahujumu miundombinu ya vyanzo vya maji na kuliagiza Jeshi la Polisi kuweka kambi katika eneo hilo, ili kudhibiti watu wanaoharibu.

Kwa upande wake Zainab Shabani mkazi wa Mhenzi amempongeza mkuu wa wilaya kwa kusimamia vyema operesheni hiyo ya kuwasaka wavamizi walioharibu vyanzo vya maji na  kusabisha wananchi kupata shida ya maji katika vijiji vyao.


No comments:

Post a Comment

Pages