HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 03, 2023

MBOMBO ATOA ONYO KALI KUELEKEA MSIMU UJAO

 

Na John Marwa 


MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Indrissa Mbombo amesema kambi waliyokaa nchini Tunisia imewafanya kuwa tayari kwa ajili ya msimu mpya wa Mashindano 2023/24.

Kikosi cha  Azam FC , kilirejea nchini juzi kikitokea nchini Tunisia ambako waliweka kambi ya wiki tatu na sasa wamerejea kujiwinda na michuano ya Ngao ya Jamii, ambapo Agust 9 watashuka dimbani kumenyana na Yanga, Mkwakwani jijini Tanga. Ikiwa ni nusu fainali ya kwanza.


Habari Mseto imepiga  stori na Mbombo alisema kambi ya Tunisia imewasaidia kupata muda wa kujamiana na wachezaji wapya jambo ambalo limewatengenezea muunganiko mzuri katika kikosi chao.


Amesema wamepata mafuzo mazuri kutoka kwa kocha Youssouph Dabo ambaye amepata muda wa kuwaandaa wachezaji wake na wako tayari kiufundi,  mbinu na utimamu wa miili yao kwa ajili ya mbiringe mbiringe za mbungi msimu ujao.



“Tumefanya mazoezi  mazuri sana, kocha amepata muda wa kunoa wachezaji wake, ameona mapungufu na kufanyia kazi, kikubwa kazi yetu ni kupambana na kutafuta matokeo chanya kwa kila mchezo.


"Tayari kocha ameshafanya majukumu yake na kazi ndogo imebaki kwake ni kujua wapi anatakiwa kufanyia kazi, kikubwa tuko tayari kwa msimu mpya na kuleta ushindani mkubwa,” amesema Mbombo.


Hata hivyo Mbombo amebainisha kuwa  wamerejea kivingine kuleta ushindani katika ligi kwa kufikia malengo yao ya kutwaa mataji yote ikiwemo kombe la Ngao ya jamii, ambalo wataanziia jijini Tanga siku chache zijazo.


Kikosi cha Azam FC kipo  kambini na watakuwa na  michezo miwili ya Kimataifa ya Kirafiki watacheza Jumamosi dhidi ya Bandari FC katika uwanja wa Azam Complex,  Chamazi.

No comments:

Post a Comment

Pages