Mtafiti wa Kilimo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Naliendele mkoani Mtwara, Zamira Matumbo (katikati) akiwaelekeza wanafunzi wa Sekondari ya Ngongo namna bora ya kilimo cha mbogamboga walipotembelea Shamba la taasisi hiyo katika Maonesho ya NaneNane ynayoendelea viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
.......................................................................................................
Dotto Mwaibale na Godwin Myovela, Lindi
TEKNOLOJIA ya mbegu bora ya zao la ufuta
inayofundishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Naliendele
mkoani Mtwara imesaidia kupatikana kwa zaidi ya Sh.Bilioni 160 katika Mkoa wa
Lindi na Mtwara baada ya kuuza ufuta katika kipindi cha msimu wa kilimo wa
mwaka 2022/ 2023.
Hayo yameelezwa na Mtafiti wa
Programu ya zao la Ufuta na Mgunduzi wa mbegu ya ufuta kutoka TARI, Naliendele
Mkoa wa Mtwara, Zabron Ngamba wakati
akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya NaneNane 2023
yanayoendelea Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
"Zao la ufuta ni la kiuchumi
katika mikoa ya Kanda ya Kusini na ndio
maana sisi TARI tumeendelea kuongeza nguvu zaidi za utafiti wa mbegu bora kwa
ajili ya kuliinua kwani soko lake ni kubwa ndani na nje ya nchi," alisema
Ngamba.
Alisema kutokana na teknolojia za mbegu
bora na ufundishaji wa kanuni za kilimo bora cha ufuta katika msimu wa kilimo
wa mwaka 2022/2023 mikoa ya Lindi na Mtwara ilipata zaidi ya Sh.Bilioni 160 kutokana na kuuza ufuta jambo ambalo linaonesha mafanikio makubwa ya kilimo cha
zao hilo.
Ngamba alisema mkulima akifuata
taratibu na kanuni za kilimo cha ufuta ile tija ya kupata tani moja ya ufuta katika
ekari mbili na nusu itapatikana hasa ikitumika mbegu aina ya Lindi 02 mkulima
anaweza kupata hata tani moja na nusu.
Ngamba anapenda kuwatoa hofu watanzania
na wakulima wa zao hilo na kuwa duniani linahitajika kwa wingi hivyo ni fursa
kubwa kuzalisha zao la ufuta kwa wingi na kulipekeka katika soko hilo ambalo
hata bei zake zinalizisha na kuwa mkulima wa anauhakika wa kupata faida na sio hasara
iwapo tu atazingatia kanuni za kilimo bora cha ufuta.
Aidha Ngamba alitumia nafasi hiyo
kuwaomba wadau mbalimbali wakiwemo wa vyama vya msingi na wasimamizi wa vyama
hivyo kuhamasisha wakulima kutumia mbegu bora na hata ikiwezekana kuwakopesha
mbegu hizo na wakisha zalisha watapeleka mazao hayo kwenye vyama hivyo na
kupata faida kwa pande zote na taifa kwa ujumla.
Ngamba aliishuru Serikali kwa
kuendelea kuwasapoti watafiti wazao hilo na mazao mengine ambapo alitoa ushauri
kwa Serikali katika kila zao linalouzwa nje ya nchi basi kiasi cha fedha
zitakazopatikana asilimia 10 itengwe kwa ajili ya kufanya utafiti jambo
litakalosaidia kuinua kilimo nchini.
Mtafiti wa Mazao ya Muhogo na Viazi
kutoka TARI Naliendele, Festo Masisila akiongelea kilimo cha viazi vitamu na
umuhimu wake alisema TARI kupitia vituo vyake vingine tayari vimesajili mbegu
za viazi vitamu 16 na ndani ya mbegu hizo kuna mbegu zenye virutubisho vyenye
vitamini A aina nane maarufu kama viazi lishe.
Alisema virutubisho hivyo vya
vitamini A vinavyotokana na viazi hivyo vinatofautiana kutokana na baina ya
mbegu na kuwa zinavumilia magonjwa na zinatumia muda mfupi kwa siku 120 tu
tayari zinapelekwa sokoni.
Alisema matumizi ya viazi hivyo
vyenye virutubisho vya vitamini A vinapotumika kwa wingi vinasaidia kukabiliana
na utapiamlo na uono havifu na hasa kwa watu ambao wapo katika makundi maalum
kama watoto wa miaka 0 hadi miaka mitano, wazee pamoja na waathirika wa virusi
vya HIV na wanapovitumia mbali ya kuongeza virutubisho hivyo pia wanaongeza
nguvu kutokana na kuwa na wanga.
Alisema chakula hicho kinaweza
kutumika kama kitafunwa cha chai, chakula cha kawaida ambacho kitasindikizwa na
maziwa yaliyogandushwa ‘mtindi’.
Alisema kutokana na umuhimu wa viazi
hivyo TARI wamekwenda mbali zaidi na kuviongeza thamani kwa kutengeneza juisi ambayo
inaweza kutumiwa na mtu yeyote wakiwemo watoto na kuwa wapo tayari kuwasidia
wadau na wajasiriamali kwenda kujifunza teknolojia ya kilimo hicho na namna ya
kuongeza thamani ya viazi hivyo.
Alisema soko la viazi hivyo ni kubwa
mno akitolea mfano mtu akivipekeka sokoni na akawakuta wenzake wanavyo vile vya
asili itabidi wasubiri kwa muda kuuza vya kwao mpaka huyo mwenye viazi lishe
avimalize na hiyo inatokana na wateja kuvigombania.
Masisila aliwaomba wananchi na
wakulima kufika banda la TARI lililopo kwenye viwanja hivyo vya NaneNane Ngongo
kwenda kujifunza teknolojia ya kilimo hicho na namna ya kupata mbegu bora.
Masisila alisema Serikali imekuwa
ikitumia fedha nyingi kuagiza kutoka nje virutubisho vya vitamini A,
kuwagharamia wataalam na wasambazaji
ambapo ametowa wito kwa wadau na makundi mengine kujikita katika
kuongeza uzalishaji wa viazi hivyo jambo litakalosaidia kupunguza matumizi ya
manone ya vitamini A kutoka nje yanchi kikubwa ni kuongeza nguvu kwa
kuwawezesha wakulima waweze kuzalisha kwa wingi viazi hivyo.
Mtafiti Mwandamizi Benadetha Kimata
kutoka TARI Naliendele ambaye ni mbobezi wa zao la Muhogo alisema zao hilo ni
la muhimu sana katika mikoa ya Kanda ya Kusini na kuwa asilimia 28 ya muhogo
unaozalishwa hapa nchini unatoka katika kanda hiyo.
Alisema zipo aina ya mbegu
mbalimbali kuna zile ambazo zinachangamoto ya magonjwa na wadudu akitolea mfano
wa zile za asili kama Albert au Mleteta ni mbegu ambazo zinaugua ugonjwa wa
mchirizi kahawia na magonjwa ya batobato ambayo yana hasara kubwa kwa mkulima
asilimia 50 hadi 100 kwa ugonjwa wa batobato na hasara yaasilimia 75 hadi 85
kwa ugonjwa wa michirizi ya kahawia.
Kimata alisema kutokana na mazao
hayo ya mbegu za asili kuwa na ukinzani mdogo wa magonjwa na uwezo wa kuzaa
kuwa na tija ndogo kiasi cha wastani wa tani 8 kwa hekta mbili na nusu
ukilinganisha na mbegu bora zilizofanyiwa utafiti na TARI zenye tija kubwa kiasi
cha tani 20 kwa wastani hadi tani 50 kwa hekta mbili na nusu ambapo wanawashauri
wakulima kutumia mbegu hizo.
Alisema mkulima akitumia mbegu hizo
bora anakuwa na nafasi nzuri ya kuwa na chakula cha kutosha katika kaya yake,
jirani na katika nchi na kupata kipato kutokana na mauzo ya muhogo na bidhaa
zake.
Alitaja bidhaa za muhogo kuwa ni
unga, wanga na kutokana na unga mkulima anaweza kutengeneza vyakula mbalimbali
kwa kutumia unga huo kama ilivyo ngano kutokana na ngano ilinayozalishwa nchini
kutotosheleza mahitaji ya watumiaji hadi kufikia hatua ya kuagizwa kutoka nje.
Kimata alisema wanapohimiza na
kuhamasisha uzianzishwaji wa viwanda vya kusindika muhogo wana lenga kuipunguzia
Selikali ya kuagiza ngano kutoka nje na watu wakatumia muhogo ambao unazalishwa
nchini kwa kutengeneza mkate, maandazi na vyakula vingine vinavyofanana na bidhaa
hizo za kuoka.
Alisema jambo hilo aliwezi kufanyika
bila ya kuwepo Sera ya Kiserikali ambayo itasaidia kuwahimiza wanao pika mikate
na mazao mengine madogo madogo yanayo okwa kuweka walau hata asimilia moja hadi
tano ya unga wanao hutumia kuzalisha bidhaa hizo wakatumia unga wa muhogo na
kuwa hilo ndilo ombi lao kwa Serikali.
No comments:
Post a Comment