HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 06, 2023

KAMA HUNA TIKETI YA SIMBA DAY UASIKATIZE LUPASO


Na John Marwa 


WAKATI yakisalia masaa kuelekea kilele cha wiki ya Simba hapo kesho, klabu ya Simba imewataka wale wote ambao hawajapata tiketi kutokatiza Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Mashabiki na wapenzi wa soka nchini watakuwa wanashuhudia tamasha kubwa la michezo barani Afrika.


Hayo yamebainishwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Power Dynamos hapo kesho.


"Tunawasisitiza wale wote ambao hawajanunua tiketi kesho wasisogee eneo la Uwanja wa Benjamin Mkapa. Kama huna tiketi kaa nyumbani Jeshi la Polisi Iinasisitiza ili kupunguza usumbufu usio wa lazima. Ambao hawana tiketi wanaweza kufatilia kupitia Azam TV.


Ahmed amewamwagia mau wanahabari na vyombo vya Habari nchini kwa kazi kubwa iliyofanyika katika kuwahamasisha wapenzi na mashabiki wa mpira nchini kununua tiketi kwa wakati.


“Tunawashukuru wanahabari kwa namna mlivyotuunga mkono tangu mwanzo mpaka hapa na hatimaye utamaduni wa kununua tiketi siku ya mwisho umeisha.


“Ni kazi kubwa ndugu zangu wanahabari mmefanya kwa kueleza faida ya kununua tiketi mapema. Simba inauthamini mchango wenu.”- amesema Ahmed Ally.

No comments:

Post a Comment

Pages